3 “‘“Mwisraeli yeyote akimchinja ng’ombe dume au mwanakondoo dume au mbuzi ndani au nje ya kambi, 4 na kukosa kumleta kwenye mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Yehova dhabihu mbele ya hema la Yehova la ibada, mtu huyo atakuwa na hatia ya damu. Ameua, naye ni lazima auawe.