2 Petro
2 Hata hivyo, kulikuja pia kuwa na manabii wasio wa kweli miongoni mwa watu, kama pia kutakavyokuwa na walimu wasio wa kweli miongoni mwenu. Hawahawa wataleta ndani kimya-kimya mafarakano yenye kuangamiza na watakana hata mmiliki aliyewanunua, wakijiletea wenyewe uangamizo wa kasi. 2 Zaidi ya hilo, wengi watafuata matendo yao ya mwenendo mlegevu, na kwa sababu ya hao njia ya kweli itasemewa kwa maneno yenye kuudhi. 3 Pia, kwa tamaa watawatumia nyinyi kujifaidi kwa maneno bandia. Lakini kuwahusu wao, hukumu ya tangu zamani za kale haiendi polepole, na uangamizo wao hausinzii.
4 Hakika ikiwa Mungu hakuacha kuadhibu malaika waliofanya dhambi, bali, kwa kuwatupa ndani ya Tartaro, aliwatia kwenye mashimo ya giza zito ili wawekwe akiba kwa ajili ya hukumu; 5 na hakuacha kuadhibu ulimwengu wa kale, bali alitunza salama Noa, mhubiri wa uadilifu, pamoja na wengine saba alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasioogopa Mungu; 6 na kwa kugeuza majiji ya Sodoma na Gomora kuwa majivu aliyahukumia adhabu, akiweka kiolezo kwa watu wasiomwogopa Mungu juu ya mambo yajayo; 7 na alimkomboa Loti mwadilifu, aliyetaabishwa sana na kujitia mno kwa watu wanaokaidi sheria katika mwenendo mlegevu— 8 kwa maana mtu huyo mwadilifu kwa yale ambayo aliona na kusikia alipokuwa akikaa miongoni mwao kutoka siku hadi siku alikuwa akitesa-tesa nafsi yake yenye uadilifu kwa sababu ya vitendo vyao vya kuasi sheria— 9 Yehova ajua jinsi ya kukomboa watu wenye ujitoaji-kimungu kutoka katika jaribu, bali kuweka akiba watu wasio waadilifu kwa ajili ya siku ya hukumu ili kukatiliwa mbali, 10 lakini, hasa, wale ambao huendelea kufuata mwili wakiwa na tamaa ya kuutia unajisi na ambao hudharau ubwana.
Wenye kuthubutu, washupavu, hawatetemekei watukufu bali husema kwa maneno yenye kuudhi, 11 lakini malaika, ijapokuwa wao ni wakubwa zaidi kwa nguvu na uwezo, hawaleti dhidi yao shtaka katika maneno yenye kuudhi, wakiwa hawafanyi hivyo kwa sababu ya kumstahi Yehova. 12 Lakini watu hawa, kama wanyama wasiofikiri waliozaliwa kiasili ili kukamatwa na kuangamizwa, hata wao, katika mambo ambayo wao hawana ujuzi na husema kwa maneno yenye kuudhi, watapatwa na uangamizo katika mwendo wao wenyewe wa uangamizo, 13 wakijikosea wenyewe kama thawabu ya utendaji wenye kosa.
Hufikiria maisha ya anasa katika wakati wa mchana kuwa raha. Wao ni madoa na mawaa, wakijitia mno katika upendezi usiozuiwa katika mafundisho yao ya udanganyifu huku wakila karamu pamoja nanyi. 14 Wana macho yenye kujaa uzinzi na yasiyoweza kuachana na dhambi, na hutongoza nafsi zisizo imara. Wana moyo uliozoezwa katika kutamani. Wao ni watoto waliolaaniwa. 15 Wakiacha pito lililo nyoofu, wameongozwa vibaya. Wamefuata pito la Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa thawabu ya utendaji wenye kosa, 16 lakini akapata karipio kwa ajili ya uhalifu wake mwenyewe wa jambo lililokuwa sahihi. Hayawani mchukua-mizigo yenye kulemea asiye na sauti, akifanya tamko kwa sauti ya mtu, alizuia mwendo wa kichaa wa huyo nabii.
17 Hawa ni mabubujiko yasiyo na maji, na ukungu uendeshwao na dhoruba yenye nguvu nyingi, na wamewekewa akiba weusi wa giza. 18 Kwa maana hutamka semi za kujivimbisha zisizo na faida, na kwa tamaa za mwili na tabia zenye ulegevu wao hutongoza wale wanaotoka tu kuponyoka kutoka kwa watu ambao hujiendesha wenyewe katika kosa. 19 Huku wao wakiwaahidi uhuru, wao wenyewe wanakuwako wakiwa watumwa wa ufisadi. Kwa maana yeyote yule anayewezwa na mwingine hufanywa mtumwa na huyu. 20 Hakika ikiwa, baada ya kuwa wameponyoka kutoka katika mambo ya unajisi ya ulimwengu kwa ujuzi sahihi juu ya Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, wanapata kujihusisha tena na mambo hayahaya na kuwezwa, hali za mwisho zimekuwa mbaya zaidi kwao kuliko zile za kwanza. 21 Kwa maana ingalikuwa bora kwao kama hawangalijua kwa usahihi pito la uadilifu kuliko baada ya kulijua kwa usahihi kugeukia mbali kutoka amri takatifu iliyokabidhiwa kwao. 22 Usemi wa mithali ya kweli umetukia kwao: “Mbwa amerudi kwenye matapiko yake mwenyewe, na nguruwe-jike aliyeoshwa kwenye kugaagaa katika matope.”