-
Kutoka 30:1-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
30 “Utajenga madhabahu ya kufukizia uvumba;+ utaijenga kwa mbao za mshita.+ 2 Itakuwa ya mraba; urefu wa mkono mmoja,* upana wa mkono mmoja, na kimo cha mikono miwili. Pembe zake zitakuwa sehemu ya madhabahu hiyo.+ 3 Utaifunika kwa dhahabu safi: sehemu yake ya juu, pande zote kuizunguka, na pembe zake; nawe utatengeneza ukingo wa dhahabu kuizunguka. 4 Pia, utaitengenezea pete mbili za dhahabu chini ya ukingo wake kwenye pande zake mbili zinazoelekeana, na pete hizo zitashikilia fito za kubebea madhabahu. 5 Tengeneza fito za mshita na kuzifunika kwa dhahabu.
-