15 Musa akamchinja, akachukua damu yake+ kwa kidole chake na kuzipaka pembe zote za madhabahu, akaitakasa madhabahu kutokana na dhambi, lakini damu iliyobaki aliimwaga kwenye msingi wa madhabahu, ili aitakase na kutoa juu yake dhabihu ya kufunika dhambi.