-
Mambo ya Walawi 11:21-24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 “‘Kati ya wadudu wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa na wanaotambaa kwa miguu yote minne, mnaweza kula tu wadudu wenye vifundo miguuni wanaoruka ardhini. 22 Hawa ndio mnaoweza kula: kila aina ya nzige wanaohama, nzige wengine wanaoliwa,+ chenene,* na panzi. 23 Wadudu wengine wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa wenye miguu minne ni chukizo kwenu. 24 Wadudu hao watawafanya msiwe safi. Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni.+
-
-
Kumbukumbu la Torati 14:8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Pia, msimle nguruwe kwa sababu ana kwato zilizopasuka lakini hacheui. Yeye si safi kwenu. Msile kamwe nyama yao wala kugusa mizoga yao.
-