-
Mwanzo 18:6, 7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Kwa hiyo Abrahamu akaenda haraka hemani na kumwambia Sara: “Fanya haraka! Chukua vipimo vitatu* vya unga laini, ukande unga huo, na kuoka mikate.” 7 Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye mifugo, akachagua ng’ombe dume mchanga, mzuri na laini. Akampa mtumishi wake, naye akafanya haraka kumtayarisha.
-
-
Mwanzo 19:3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Lakini akawasihi sana hivi kwamba wakaingia pamoja naye ndani ya nyumba yake. Kisha akawaandalia karamu, akaoka mikate isiyo na chachu, nao wakala.
-