8 Kisha akajenga chumba cha Patakatifu Zaidi;+ urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono 20, na upana wake ulikuwa mikono 20. Akaifunika kwa talanta 600 za dhahabu bora.+ 9 Uzito wa dhahabu iliyotumiwa kutengenezea misumari ulikuwa shekeli 50; naye alifunika vyumba vya darini kwa dhahabu.