-
1 Wafalme 18:23, 24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 Na watupatie ng’ombe dume wachanga wawili, kisha wachague ng’ombe dume mmoja mchanga na kumkata vipandevipande na kuviweka juu ya kuni, lakini wasiwashe moto. Nitamtayarisha ng’ombe dume mchanga wa pili na kumweka juu ya kuni, lakini sitawasha moto. 24 Kisha mtaliita jina la mungu wenu,+ nami nitaliita jina la Yehova. Mungu atakayejibu kwa moto, atathibitisha kwamba yeye ndiye Mungu wa kweli.”+ Ndipo watu wote wakasema: “Jambo unalosema ni jema.”
-