-
Isaya 36:4-10Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Basi Rabshake akawaambia: “Tafadhali, mwambieni hivi Hezekia: ‘Mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, anauliza, “Ujasiri wako unategemea msingi gani?+ 5 Unasema, ‘Nina mbinu na nguvu za kupigana vita,’ lakini hayo ni maneno matupu. Unamtumaini nani, hivi kwamba unathubutu kuniasi?+ 6 Tazama! Unautumaini msaada wa utete huu uliopondeka, Misri, ambao mtu yeyote akiuegemea utamchoma kiganja na kukitoboa. Hivyo ndivyo Farao mfalme wa Misri alivyo kwa wote wanaomtumaini.+ 7 Nawe ukiniambia, ‘Tunamtumaini Yehova Mungu wetu,’ je, si yeye ndiye ambaye mahali pake pa juu na madhabahu zake zimeondolewa na Hezekia,+ huku akiwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuinama mbele ya madhabahu hii’?”’+ 8 Basi sasa, tafadhali, fanya mkataba huu pamoja na bwana wangu mfalme wa Ashuru:+ nitakupa farasi 2,000 ikiwa unaweza kupata wapanda farasi wa kutosha idadi hiyo. 9 Basi, unawezaje kumzuia hata gavana mmoja aliye mdogo zaidi kati ya watumishi wa bwana wangu, huku ukiitumaini nchi ya Misri ili upate magari ya vita na wapanda farasi? 10 Sasa je, nimepanda kuja kuishambulia nchi hii ili kuiharibu bila kupewa idhini na Yehova? Yehova mwenyewe aliniambia, ‘Panda uende kuishambulia nchi hii na kuiharibu.’”
-