21 Halafu nikachukua kile kitu cha dhambi mlichokitengeneza, yule ndama,+ na kumteketeza kwa moto; nikamponda na kumsagasaga kabisa mpaka akawa laini kama mavumbi, nami nikayatupa mavumbi hayo katika kijito kinachotiririka kutoka mlimani.+
29 Kwa maana najua vizuri kwamba baada ya kifo changu hakika mtatenda maovu+ na kuacha njia ambayo nimewaamuru ninyi. Na bila shaka mtapatwa na msiba+ siku zijazo, kwa sababu mtatenda maovu machoni pa Yehova, nanyi mtamkasirisha kwa kazi za mikono yenu.”