-
2 Wafalme 11:9-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Wakuu wa mamia+ wakafanya sawasawa na alivyoamuru kuhani Yehoyada. Basi kila mmoja wao akachukua wanaume wake waliokuwa na zamu siku ya Sabato, pamoja na wale ambao hawakuwa na zamu siku ya Sabato, wakaja kwa kuhani Yehoyada.+ 10 Kisha kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao za mviringo zilizokuwa za Mfalme Daudi, ambazo zilikuwa katika nyumba ya Yehova. 11 Na walinzi wa jumba la mfalme+ wakasimama mahali pao, kila mmoja akiwa na silaha zake mikononi, kuanzia upande wa kulia wa nyumba mpaka upande wa kushoto wa nyumba, kando ya madhabahu,+ na kando ya nyumba hiyo, kumzunguka mfalme pande zote. 12 Kisha Yehoyada akamtoa nje mwana wa mfalme+ na kumvika taji na Ushahidi,*+ wakamweka kuwa mfalme na kumtia mafuta. Wakaanza kupiga makofi na kusema: “Mfalme na aishi muda mrefu!”+
-