4 Baada ya muda Yehoahazi akamsihi Yehova amwonyeshe kibali, naye Yehova akamsikiliza, kwa maana alikuwa ameona jinsi mfalme wa Siria alivyowakandamiza Waisraeli.+ 5 Basi Yehova akawapa Waisraeli mwokozi+ ili awaokoe kutoka mikononi mwa Wasiria, na Waisraeli wakakaa katika nyumba zao kama awali.