-
Hesabu 22:4-6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Basi Wamoabu wakawaambia wazee wa Midiani:+ “Sasa umati huu utaramba eneo letu lote kama ng’ombe dume anavyokula nyasi shambani.”
Balaki mwana wa Sipori ndiye aliyekuwa mfalme wa Moabu wakati huo. 5 Aliwatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori huko Pethori,+ karibu na Mto Efrati katika nchi yake. Alimwambia hivi: “Sasa, kuna watu ambao wametoka Misri. Wamejaa kila mahali duniani,*+ na wanakaa papa hapa karibu nami. 6 Basi, tafadhali, njoo uwalaani watu hawa kwa niaba yangu,+ kwa maana wana nguvu kuliko mimi. Huenda nikawashinda na kuwafukuza kutoka nchini, kwa maana najua vema kwamba yule unayembariki amebarikiwa na yule unayemlaani amelaaniwa.”
-