17 Na katika mikoa yote na majiji yote, popote ambapo agizo la mfalme na sheria yake ilifika, Wayahudi walifurahi na kushangilia, wakafanya karamu na kusherehekea. Watu wengi wa mataifa yaliyokuwa nchini walikuwa wakijitangaza kuwa Wayahudi,+ kwa maana waliwaogopa Wayahudi.