-
Esta 6:11, 12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Basi Hamani akachukua mavazi hayo na farasi, akamvisha Mordekai+ na kumtembeza katika uwanja wa jiji akiwa juu ya farasi na kutangaza kwa sauti mbele yake: “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu!” 12 Baadaye Mordekai akarudi kwenye lango la mfalme, lakini Hamani akaenda haraka nyumbani kwake, akiomboleza akiwa amefunika kichwa chake.
-