-
1 Wafalme 21:8-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Basi Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akazipiga muhuri wa Ahabu+ na kuzituma barua hizo kwa wazee+ na wakuu walioishi katika jiji la Nabothi. 9 Aliandika hivi katika barua hizo: “Tangazeni watu wafunge, halafu mketisheni Nabothi mbele ya watu. 10 Nanyi muwaketishe watu wawili wasiofaa kitu mbele yake ili watoe ushahidi dhidi yake,+ wakisema, ‘Umemtukana Mungu na mfalme!’+ Kisha mtoeni nje na kumuua kwa kumpiga mawe.”+
11 Basi watu wa jiji lake, wazee na wakuu walioishi katika jiji lake, wakafanya kama ilivyoandikwa katika barua ambazo Yezebeli aliwatumia.
-
-
Yeremia 38:4, 5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Wakuu wakamwambia mfalme: “Tafadhali agiza mtu huyu auawe,+ kwa maana hivyo ndivyo anavyoidhoofisha mioyo* ya wanajeshi waliobaki jijini, na pia ya watu wote, kwa kuwaambia maneno hayo. Kwa maana mtu huyu hawatakii amani watu hawa, bali msiba.” 5 Mfalme Sedekia akajibu: “Tazama! Yuko mikononi mwenu, kwa maana mfalme hawezi kufanya jambo lolote ili kuwazuia.”
-