-
2 Wafalme 18:28-35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 Kisha Rabshake akasimama na kusema hivi kwa sauti kubwa kwa lugha ya Wayahudi: “Sikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru.+ 29 Mfalme anasema hivi: ‘Msikubali Hezekia awadanganye, kwa maana hawezi kuwaokoa kutoka mikononi mwangu.+ 30 Na msikubali Hezekia awafanye mumtumaini Yehova mkisema: “Kwa hakika Yehova atatuokoa, na jiji hili halitatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.”+ 31 Msimsikilize Hezekia, kwa maana mfalme wa Ashuru anasema hivi: “Fanyeni amani pamoja nami na mjisalimishe,* na kila mmoja wenu atakula matunda ya mzabibu wake mwenyewe na matunda ya mtini wake mwenyewe na kunywa maji kutoka katika tangi lake mwenyewe, 32 mpaka nitakapokuja na kuwapeleka katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe,+ nchi yenye nafaka na divai mpya, nchi yenye mikate na mashamba ya mizabibu, nchi yenye mizeituni na asali. Ndipo mtakapoishi, nanyi hamtakufa. Msimsikilize Hezekia, kwa maana anawapotosha kwa kusema, ‘Yehova atatuokoa.’ 33 Je, kuna mungu yeyote kati ya miungu ya mataifa ambaye amewahi kuiokoa nchi yake kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru? 34 Iko wapi miungu ya Hamathi+ na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu,+ Hena, na Iva? Je, imeokoa Samaria kutoka mikononi mwangu?+ 35 Ni mungu yupi kati ya miungu yote ya nchi mbalimbali ambaye ameokoa nchi yake kutoka mikononi mwangu, hivi kwamba Yehova aokoe Yerusalemu kutoka mikononi mwangu?”’”+
-