5 Kwa hiyo walitawanyika kwa sababu hakukuwa na mchungaji;+ walitawanyika na kuwa chakula cha kila mnyama wa mwituni. 6 Kondoo wangu waliendelea kutangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu; kondoo wangu walitawanyika kotekote duniani, na hakuna aliyewatafuta au kujitahidi kuwapata.