-
Ezekieli 1:27, 28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
27 Nami nikaona kitu kinachong’aa kama mchanganyiko wa dhahabu na fedha,+ kilichokuwa kama moto unaong’aa kutoka kwenye kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kwenda juu; na kutoka kwenye kiuno chake kwenda chini, nikaona kitu kilichofanana na moto.+ Kulikuwa na mwangaza mkali kumzunguka pande zote 28 kama wa upinde wa mvua+ katika mawingu siku ya mvua. Hivyo ndivyo mwangaza uliozunguka pande zote ulivyoonekana. Ulikuwa kama mwonekano wa utukufu wa Yehova.+ Nilipouona, nikaanguka chini kifudifudi na kuanza kusikia sauti ya mtu akizungumza.
-