-
1 Samweli 2:13, 14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Hivi ndivyo walivyofanya kuhusu vitu vilivyoletwa na watu ambavyo vilikuwa haki ya makuhani:+ Kila mara mtu yeyote alipokuwa akitoa dhabihu, mtumishi wa kuhani alikuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake nyama ilipokuwa ikichemka, 14 naye aliutia kwa nguvu ndani ya beseni, chungu cha kupikia chenye mikono miwili, sufuria kubwa, au chungu cha kupikia chenye mkono mmoja. Nyama yoyote iliyoinuliwa na uma huo, ilichukuliwa na kuhani. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakiwatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo.
-