64 “Yehova atawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia mpaka mwisho mwingine wa dunia,+ na huko mtalazimika kuabudu miungu ya miti na mawe, ambayo wala ninyi wala mababu zenu hamwijui.+
12 Theluthi yenu moja watakufa kwa ugonjwa hatari au kuangamia kwa njaa kali miongoni mwenu. Na theluthi nyingine watauawa kwa upanga kuwazunguka pande zote.+ Nami nitaitawanya theluthi ya mwisho kila upande,* nami nitauchomoa upanga ili kuwakimbiza.+