5 Basi, wakafika ng’ambo ya bahari na kuingia katika eneo la Wagerasene.+ 2 Mara tu Yesu alipotoka kwenye mashua akakutana na mtu mwenye roho mwovu akitoka makaburini. 3 Alikuwa akikaa makaburini, na kufikia wakati huo hakuna mtu yeyote aliyeweza kumfunga kabisa hata kwa mnyororo.