-
Luka 23:20-25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Pilato akawapazia sauti tena, kwa sababu alitaka kumfungua Yesu.+ 21 Ndipo wakaanza kupiga kelele, wakisema: “Atundikwe mtini! Atundikwe mtini!”*+ 22 Akawaambia mara ya tatu: “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Mimi sikuona jambo lolote linalofanya astahili kifo; kwa hiyo nitamwadhibu kisha nimfungue.” 23 Lakini wakazidi kusisitiza, wakidai kwa sauti kubwa, kwamba auawe,* na sauti zao zikashinda.+ 24 Basi Pilato akaamua kutimiza dai lao. 25 Akamfungua yule mtu waliyemtaka, ambaye alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya uchochezi na mauaji, lakini akamkabidhi Yesu mikononi mwao ili wamtendee wanavyopenda.
-