-
Mathayo 9:16, 17Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
16 Hakuna mtu anayeshona kiraka cha kitambaa kipya juu ya vazi la nje la zamani; kwa maana hicho kitambaa kipya kitatoka kwenye hilo vazi nalo litararuka vibaya zaidi.+ 17 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vya divai vilivyochakaa. Wakifanya hivyo, viriba hivyo vitapasuka na divai itamwagika navyo viriba vitaharibika. Lakini watu huweka divai mpya katika viriba vipya vya divai, na vitu vyote viwili huhifadhiwa.”
-
-
Luka 5:36-38Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
36 Pia, akawapa mfano: “Hakuna mtu anayekata kiraka cha vazi jipya la nje na kukishona kwenye vazi la zamani. Akifanya hivyo, kiraka kipya hurarua vazi la zamani na kiraka kipya hakilingani na vazi la zamani.+ 37 Pia, hakuna mtu anayeweka divai mpya katika viriba vya divai vilivyochakaa. Akifanya hivyo, divai mpya itavipasua viriba, nayo itamwagika na viriba vitaharibika. 38 Lakini divai mpya lazima iwekwe katika viriba vipya vya divai.
-