-
Mathayo 14:19-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Akauagiza umati uketi kwenye nyasi. Kisha akachukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akatoa baraka+ na baada ya kuimega mikate, akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakaugawia umati. 20 Basi wote wakala wakashiba, nao wakakusanya vipande vilivyobaki, wakajaza vikapu 12.+ 21 Sasa wale waliokula walikuwa wanaume karibu 5,000, na pia wanawake na watoto wadogo.+
-
-
Marko 6:39-44Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
39 Akawaagiza watu wote waketi katika vikundi kwenye nyasi.+ 40 Basi wakaketi katika vikundi vya watu 100 na vya watu 50. 41 Akachukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni akatoa baraka.+ Kisha akaimega mikate na kuanza kuwapa wanafunzi ili wawape watu, naye akawagawanya wale samaki wawili kwa ajili ya watu wote. 42 Basi wote wakala wakashiba, 43 nao wakakusanya vipande vilivyobaki na kujaza vikapu 12, bila kuhesabu samaki.+ 44 Wale waliokula mikate hiyo walikuwa wanaume 5,000.
-
-
Luka 9:14-17Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Kwa kweli, kulikuwa na karibu wanaume 5,000. Lakini akawaambia wanafunzi wake: “Waambieni waketi katika vikundi vya watu hamsini hamsini.” 15 Wakafanya hivyo, na kila mtu akaketi. 16 Akachukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni na kuvibariki. Kisha akavimega, akaanza kuwapa wanafunzi ili wawape watu. 17 Basi wote wakala wakashiba, nao wakakusanya chakula kilichobaki na kujaza vikapu 12.+
-