-
Mambo ya Walawi 24:3, 4Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Katika hema la mkutano, nje ya pazia lililo karibu na sanduku la ushahidi, Haruni atahakikisha kwamba taa hizo zinawaka daima kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Yehova. Hiyo ni sheria ya kudumu katika vizazi vyenu vyote. 4 Haruni anapaswa kupanga taa hizo kwa utaratibu kwenye kinara cha taa+ cha dhahabu safi mbele za Yehova daima.
-