-
Mwanzo 19:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Wale malaika wawili wakafika Sodoma jioni, na Loti alikuwa ameketi katika lango la Sodoma. Loti alipowaona, akasimama ili awapokee, akainama chini kifudifudi.+ 2 Naye akasema: “Tafadhali, bwana zangu, tafadhali, karibuni nyumbani mwangu mimi mtumishi wenu, mlale hapa usiku wa leo, nasi tuioshe miguu yenu. Kisha mnaweza kuamka asubuhi na mapema na kuendelea na safari yenu.” Wakamwambia: “Hapana, tutakaa usiku kucha kwenye uwanja wa jiji.” 3 Lakini akawasihi sana hivi kwamba wakaingia pamoja naye ndani ya nyumba yake. Kisha akawaandalia karamu, akaoka mikate isiyo na chachu, nao wakala.
-