Ayubu
19 Ayubu akajibu:
4 Na ikiwa kwa kweli nilifanya kosa,
Ni kosa langu mimi mwenyewe.
5 Ikiwa mnasisitiza kujikweza juu yangu,
Mkidai kwamba mna haki ya kunishutumu,
6 Basi, jueni kwamba Mungu ndiye amenipotosha,
Naye ameninasa katika wavu wake wa kuwindia.
7 Tazameni! Naendelea kulia kwa sauti, ‘Ukatili!’ lakini sijibiwi;+
Naendelea kulilia msaada, lakini hakuna haki.+
9 Amenivua utukufu wangu
Na kunivua taji kichwani.
10 Hunibomoa kila upande na kuniangamiza;
Anang’oa tumaini langu kama mti.
12 Majeshi yake hukusanyika na kunizingira,
Nayo hupiga kambi kuzunguka hema langu.
16 Ninamwita mtumishi wangu, lakini hajibu;
Namsihi kwa kinywa changu anihurumie.
18 Hata watoto wachanga wananidharau;
Ninaposimama, wanaanza kunifanyia mzaha.
20 Mifupa yangu inashikamana na ngozi yangu na mwili wangu,+
Nami ninaponyoka kwa ngozi ya meno yangu.
21 Nionyesheni rehema, rafiki zangu, nionyesheni rehema,
Kwa maana mkono wa Mungu mwenyewe umenigusa.+
23 Laiti maneno yangu yangeandikwa,
Laiti yangeandikwa katika kitabu!
24 Laiti yangechongwa milele kwenye mwamba,
Kwa kalamu ya chuma na risasi!
26 Baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi,
Nikiwa bado hai, nitamwona Mungu,
27 Ambaye mimi mwenyewe nitamwona,
Ambaye macho yangu mwenyewe yatamwona, si ya mwingine.+
Lakini ndani kabisa ninahisi nimelemewa!*
28 Kwa maana mnauliza, ‘Tunamtesa kwa njia gani?’+
Kwa maana mimi ndiye mzizi wa tatizo hili.