Ayubu
40 Yehova akaendelea kumjibu Ayubu:
2 “Je, mtu anayetafuta makosa anapaswa kushindana na Mweza-Yote?+
Acha yule anayetaka kumkaripia Mungu ajibu.”+
3 Ayubu akamjibu Yehova:
Nitakujibu nini?
Ninafunika kinywa changu kwa mkono.+
5 Niliongea mara moja, lakini sitajibu tena;
Mara mbili, lakini sitaongea tena.”
6 Kisha Yehova akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba ya upepo:+
8 Je, utatilia shaka* haki yangu?
Je, utanishutumu ili uwe mwadilifu?+
9 Je, una mkono wenye nguvu kama mkono wa Mungu wa kweli,+
Au je, sauti yako inaweza kunguruma kama yake?+
10 Tafadhali, jipambe kwa utukufu na ukuu;
Jivike heshima na fahari.
11 Mwaga ghadhabu ya hasira yako;
Mtazame kila mwenye kiburi, umshushe chini.
12 Mtazame kila mwenye kiburi, umnyenyekeze,
Na uwakanyage waovu mahali wanaposimama.
13 Wafiche wote mavumbini;
Wafunge* mahali palipofichika,
14 Ndipo hata mimi nitakapokiri mbele yako*
Kwamba mkono wako wa kulia unaweza kukuokoa.
15 Tazama, huyu ni Behemothi* niliyemuumba kama nilivyokuumba.
Yeye hula majani kama ng’ombe dume.
16 Tazama nguvu zilizo kiunoni mwake
Na nguvu zilizo katika misuli ya tumbo lake!
17 Huukaza mkia wake kama mwerezi;
Kano za mapaja yake zimefumwa pamoja.
18 Mifupa yake ni mabomba ya shaba;
Miguu yake ni kama fito za chuma kilichofuliwa.
19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu;
Ni Muumba wake tu anayeweza kumkaribia kwa upanga wake.
20 Kwa maana milima huzalisha chakula kwa ajili yake,
Ambako wanyama wote wa mwituni hucheza.
21 Hulala chini ya miti ya miyungiyungi,
Kwenye kivuli cha matete mahali penye umajimaji.
23 Mto unaposukasuka, yeye hashtuki.
Haogopi hata maji ya Yordani+ yakifurika kinywani mwake.