Ayubu
13 “Naam, jicho langu limeona hayo yote,
Sikio langu limesikia na kuyaelewa.
2 Mnayojua, mimi pia nayajua;
Mimi si duni kwenu.
6 Tafadhali, sikilizeni hoja zangu,
Na msikilize ninapojitetea kwa midomo yangu.
7 Je, mtasema mambo yasiyo ya haki kwa niaba ya Mungu,
Na je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa ajili yake?
9 Je, mambo yatawaendea vyema akiwachunguza?+
Je, mtamdanganya kama mnavyomdanganya mwanadamu anayeweza kufa?
11 Je, adhama yake mwenyewe haitawaogopesha
Na hofu yake haitawaangukia?
13 Nyamazeni mbele yangu, ili niongee.
Kisha na yanipate yatakayonipata!
16 Ndipo atakapokuwa wokovu wangu,+
Kwa maana hakuna mtu aliyemkataa Mungu* anayeweza kuja mbele zake.+
17 Sikilizeni kwa makini neno langu;
Sikilizeni tangazo langu.
18 Sasa tazameni, nimetayarisha kesi yangu;
Najua sina kosa.
19 Ni nani atakayepambana nami?
Nitakufa, ikiwa nitanyamaza!*
22 Niite nami nitakujibu,
Au acha nizungumze, nawe unijibu.
23 Nimefanya makosa na dhambi gani?
Nifunulie kosa langu na dhambi yangu.
25 Je, utajaribu kulitisha jani linalopeperushwa na upepo
Au kuyakimbiza majani makavu?
26 Kwa maana unaendelea kuandika mashtaka makali dhidi yangu,
Nawe unanifanya niwajibike kwa sababu ya dhambi nilizofanya nilipokuwa kijana.
27 Umeitia miguu yangu katika mikatale,
Unavichunguza kwa makini vijia vyangu vyote,
Nawe unafuata kila wayo wa mguu wangu.