Nahumu
3 Ole kwa jiji la umwagaji wa damu!
Limejaa kabisa udanganyifu na unyang’anyi.
Halikosi kamwe mawindo!
2 Kuna sauti ya mjeledi na mlio wa magurudumu,
Farasi anayekimbia kasi na gari la vita linalorukaruka.
3 Mpanda farasi aliye juu ya farasi, upanga unaomweka, na mkuki unaometameta,
Umati wa watu waliouawa na marundo ya maiti
—Maiti hazihesabiki.
Wanaendelea kujikwaa juu ya maiti.
4 Yote hayo ni kwa sababu ya matendo mengi ya ukahaba yaliyotendwa na huyo kahaba,
Aliye mrembo na mwenye kuvutia, bimkubwa wa uchawi,
Anayeyanasa mataifa kwa ukahaba wake na familia kwa uchawi wake.
5 “Tazama! Niko dhidi yako,”* asema Yehova wa majeshi,+
“Nitainua nguo yako juu na kufunika uso wako;
Nitayafanya mataifa yaone uchi wako,
Na falme zione aibu yako.
Ni nani atakayelihurumia?’
Nitakutafutia wapi wafariji?
8 Je, wewe ni bora kuliko jiji la No-amoni,*+ lililoketi kando ya mifereji ya Nile?+
Maji yalilizunguka;
Utajiri wake ulikuwa bahari na ukuta wake ulikuwa bahari.
9 Nchi ya Ethiopia ilikuwa chanzo cha nguvu zake zisizo na mipaka, pia Misri.
Putu+ na Walibya walikusaidia.+
Watoto wake pia walipondwa-pondwa katika kila pembe ya barabara.
Walipiga kura ili kuwauza wanaume wake wanaoheshimiwa,
Na wanaume wake wote wakuu wamefungwa kwa pingu.
Utatafuta kimbilio kutoka kwa adui.
12 Ngome zako zote ni kama mitini yenye tini za kwanza zilizoiva;
Zikitikiswa, zitaanguka kinywani mwa walaji walafi.
13 Tazama! Wanajeshi wako ni kama wanawake kati yako.
Malango ya nchi yako yatakuwa wazi kabisa kwa ajili ya maadui wako.
Moto utateketeza kabisa makomeo ya malango yako.
14 Teka maji kabla hujazingirwa!+
Imarisha ngome zako.
Shuka chini kwenye matope na kukanyagakanyaga udongo wa mfinyanzi;
Chukua chombo cha kufyatulia matofali.
15 Hata huko moto utakuteketeza kabisa.
Upanga utakukatakata.+
Utakutafuna kama nzige wachanga wanavyofanya.+
Ongezeka sana kama nzige wachanga!
Naam, ongezeka sana kama nzige!
16 Umezidisha wafanyabiashara wako kuliko nyota za mbinguni.
Nzige mchanga hujivua ngozi kisha huruka na kwenda zake.
17 Walinzi wako ni kama nzige,
Na maofisa wako ni kama kundi la nzige.
Wanapiga kambi katika mazizi ya mawe siku yenye baridi,
Lakini jua linapowaka, wao huruka na kwenda zao;
Na hakuna yeyote anayejua mahali walipo.
18 Wachungaji wako wanasinzia, Ee mfalme wa Ashuru;
Wakuu wako wanakaa katika makao yao.
Watu wako wametawanyika milimani,
Na hakuna yeyote anayewakusanya pamoja.+
19 Msiba wako hauna kitulizo.
Jeraha lako haliwezi kuponywa.