Wimbo wa Sulemani
2 “Kama yungiyungi katikati ya miiba
Ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya mabinti.”
3 “Kama mtofaa kati ya miti ya msituni,
Ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wana.
Natamani sana kukaa katika kivuli chake,
Na tunda lake ni tamu kinywani mwangu.
Msijaribu kuamsha au kuchochea upendo ndani yangu mpaka utakapoamka wenyewe.+
8 Sauti ya mpenzi wangu!
Tazama! Ndiye yule anakuja,
Akipanda milima, akirukaruka juu ya vilima.
9 Mpenzi wangu ni kama swala, kama paa dume mchanga.+
Yule pale, amesimama nyuma ya ukuta wetu,
Akichungulia madirishani,
Akitazama kupitia viunzi vya madirisha.
10 Mpenzi wangu anaongea, ananiambia:
‘Inuka, mpenzi wangu,
Mrembo wangu, njoo twende zetu.
11 Angalia, majira ya baridi* yamepita.
Mvua zimekwisha na kwenda zake.
Inuka, mpenzi wangu, njoo.
Mrembo wangu, njoo twende zetu.
14 Ewe njiwa wangu, kwenye mapango ya miamba,+
Kwenye mashimo ya mlimani,
Acha nikuone na kusikia sauti yako,+
Kwa maana sauti yako inavutia na umbo lako linapendeza.’”+
15 “Tukamatieni mbweha,
Mbweha wadogo wanaoharibu mashamba ya mizabibu,
Kwa maana mashamba yetu ya mizabibu yamechanua.”