Sura 42
Yesu Akemea Mafarisayo
IKIWA ni kwa nguvu za Shetani yeye anafukuza roho waovu, Yesu anatoa hoja yake, basi Shetani amegawanyika dhidi yake mwenyewe. “Ama nyinyi mfanye mti uwe mzuri sana na tunda lao liwe zuri sana,” yeye anaendelea kusema, “au mfanye mti uoze na tunda lao lioze; kwa maana mti unajulikana kwa tunda lao.”
Ni upumbavu kutoa shtaka la kwamba tunda jema la kufukuza roho waovu linatokea kwa sababu Yesu anatumikia Shetani. Ikiwa tunda ni zuri sana, mti hauwezi kuwa umeoza. Kwa upande ule mwingine, tunda lililooza la Mafarisayo la mashtaka ya upuuzi na upinzani usio na msingi kwa Yesu ni uthibitisho wa kwamba wao wenyewe wameoza. “Wazao wa nyoka wenye sumu,” Yesu anapaaza sauti, “mnaweza kunenaje mambo mema, hali nyinyi wenyewe ni waovu? Kwa maana kinywa hunena kutokana na utele wa moyo.”
Kwa kuwa maneno yetu yanaonyesha hali ya mioyo yetu, tunayosema yanaandaa msingi wa hukumu. “Maana nawaambia nyinyi,” Yesu anasema, “kwa kila usemi usioweza kuleta faida ambao wanadamu wananena, wao watatoa sababu kuuhusu katika Siku ya Hukumu; kwa maana kwa maneno yenu nyinyi mtatangazwa kuwa waadilifu, na kwa maneno yenu mtashutumiwa vikali.”
Zijapokuwa kazi zote za ajabu za Yesu, waandishi na Mafarisayo wanaomba hivi: “Mwalimu, sisi tunataka kuona ishara moja kutoka kwako wewe.” Ingawa huenda watu hawa hasa kutoka Yerusalemu hawajajionea wao wenyewe miujiza yake, upo ushahidi usiopingika wa wale waliojionea kwa macho yao wenyewe miujiza hiyo. Kwa hiyo Yesu anawaambia viongozi hao Wayahudi: “Kizazi kiovu na chenye uzinzi kinaendelea kutafuta ishara, lakini hakuna ishara kitakayopewa isipokuwa ishara ya Yona yule nabii.”
Akieleza analomaanisha, Yesu anaendelea kusema: “Sawa na vile Yona alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa sana michana mitatu na siku tatu. Ndivyo Mwana wa binadamu atakavyokuwa katika moyo wa dunia michana mitatu na siku tatu.” Baada ya kumezwa na samaki huyo, Yona alitoka nje kama kwamba amefufuliwa, hivyo Yesu anatabiri kwamba yeye atakufa na siku ya tatu atainuliwa akiwa hai. Hata hivyo, viongozi hao Wayahudi, hata Yesu anapofufuliwa baadaye wanaikataa “ishara ya Yona.”
Hivyo Yesu anasema kwamba watu wa Ninawi waliotubu kwa kusikia mahubiri ya Yona watainuka katika hukumu kushutumu vikali Wayahudi wanaomkataa Yesu. Vivyo hivyo, yeye anatokeza ulinganifu pamoja na malkia wa Sheba, aliyekuja kutoka miisho ya dunia asikie hekima ya Solomoni naye akastaajabishwa na aliyoona na kusikia. “Lakini, tazama!” Yesu anasema, “kitu fulani kilicho zaidi ya Solomoni kipo hapa.”
Ndipo Yesu anapotoa kielezi cha mwanamume anayetokwa na roho mchafu. Hata hivyo, mwanamume huyo hajazi utupu uliobaki kwa mambo mema, kwa hiyo anapagawa na roho saba waovu zaidi. “Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia na kizazi hiki kiovu,” Yesu anasema. Taifa la Israeli lilikuwa limesafishwa uchafu na likapata maumbo mapya—kama mwondoko wa muda wa roho mchafu. Lakini kukataa manabii wa Mungu kwa taifa hilo, kukifikia upeo kwa kumpinga Kristo mwenyewe, kwafunua hali mbovu lililo nayo kuwa mbaya zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni.
Wakati Yesu anapoendelea kunena, mamaye na ndugu zake wanafika na kusimama kwenye ukingo wa umati wa watu. Kwa hiyo mtu fulani anasema: “Tazama! Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wakitafuta kunena na wewe.”
“Ni nani mama yangu, na ni nani ndugu zangu?” Yesu anauliza. Akinyosha mkono wake kuelekea wafuasi wake, yeye anasema: “Tazama! Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu yeyote anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye ndugu, na dada, na mama yangu.” Kwa njia hiyo Yesu anaonyesha kwamba hata viwe ni vyenye thamani kama nini vifungo vinavyomfunganisha yeye na watu wa ukoo wake, wenye thamani hata zaidi ni uhusiano wake na wafuasi wake. Mathayo 12:33-50, NW; Marko 3:31-35; Luka 8:19-21.
▪ Mafarisayo wanashindwaje kufanya “mti” na “tunda” lao pia liwe zuri?
▪ “Ishara ya Yona” ni nini, nayo baadaye inakataliwaje?
▪ Taifa la Israeli la karne ya kwanza likoje kama mwanamume aliyetokwa na roho mchafu?
▪ Yesu anakaziaje uhusiano wake wa karibu pamoja na wanafunzi wake?