Alikuwa na Imani Isiyotikisika
Kwa miaka miwili Renata mwenye umri wa miaka 14 wa nchi ya Brazili alikuwa amesumbuliwa na kansa (donda baya) ya mifupa katika goti lake la kushoto. Alipokatwa mguu na kupewa matibabu ya kutumia madini ya kobalti hakupona kabisa, bali hiyo iliahirisha kifo chake tu. Dhamiri ya Kikristo ya Renata ilimkataza kukubali kutiwa damu mishipani, ijapokuwa daktari alishikilia kauli ya kwamba anapaswa kutiwa damu. Kabla ya kuingia hospitali safari yake ya mwisho, daktari huyo na mkunga wa kike walienda nyumbani kwa akina Renata kumwona.
“Mimi nakubali kurudi hospitali ikiwa Dakt. —— ataniahidi kwamba hatanitajia damu tena. Nimechoka kuambiwa-ambiwa nitiwe damu,” akatamka Renata.
Daktari alikubali na akaongeza kusema kwamba, ingawa huenda Renata akawa anaishi katika dakika za mwisho za uhai wake, alikuwa na imani isiyotikisika.
Wakati wa miezi minane ya mwisho Renata hakuweza kulala kwa sababu ya maumivu makali sana. Wakati ulipofika wa kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, alilia na kusema: “Kama tu ningeweza kusema na kila mtu ningemwambia, ‘Tumia miguu yako sana kwa kadiri uwezavyo. Labda kesho hutaweza kutembea wala kumfanyia Yehova kazi. Usikose kuyahudhuria makusanyiko yanayokuwako!’”
Renata alitoa sala za daima. Siku moja mama yake akamsikia kwa mbali akisali hivi: “Yehova, mimi najua sitapata nafuu kamwe. Madaktari hawawezi kuniponya, lakini Wewe unaweza. Lakini najua kwamba wakati wa kufanya hivyo haujafika; ni katika Taratibu Mpya tu. Lakini tafadhali usiache nivimbe tena; au sivyo, mama atashindwa kunipeleka kwenye haja (msalani).”
Wakati wengine, kutia ndani mama yake, walipolia wakiwa mbele yake, Renata alikuwa akiwatia moyo wawe wenye nguvu katika imani. Mama yake anaandika hivi: “Lakini nakumbuka kwamba siku moja baada ya yeye kukatwa mguu, mkunga mmoja (wa hospitali) alimwambia Renata, ‘Uliwezaje kuwa mchangamfu namna hiyo ulipokuwa juu ya meza ya upasuaji? Ni vizuri kwamba utapata mguu wa bandia, au waonaje?’ Renata akajibu, ‘Hapana, mimi natazamia kupata mguu wenye nyama na damu, ambao Yehova Mungu atanipa katika Taratibu Mpya.’”
[Blabu katika ukurasa wa 19]
Alipolazwa hospitali akae huko, Renata alihimiza hivi: “Usikose kuyahudhuria makusanyiko yanayokuwako!”