Mazungumzo Ya Familia
Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?
Soma Esta 5:9–6:14. Ni mambo gani matatu katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini, na ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.
1. ․․․․․
2. ․․․․․
3. ․․․․․
ZUNGUMZENI PAMOJA:
Kwa nini Hamani alimchukia Mordekai?
Dokezo: Soma Esta 5:9.
Kiburi kilimfanya Hamani afikie mkataa gani wenye makosa?
Dokezo: Soma Esta 6:6.
Ni nini kilichompata Hamani?
Dokezo: Soma Esta 7:9, 10.
Ni kwa njia gani unaweza kuepuka kuwa kama Hamani?
Dokezo: Soma Methali 16:18, 19; Yakobo 4:6.
UTENDAJI WA FAMILIA:
Someni simulizi hilo la Biblia pamoja. Ikiwezekana, mmoja asome sehemu ya msimuliaji, wa pili asome sehemu ya Hamani, wa tatu asome sehemu ya Zereshi na watumishi, na wanne asome sehemu ya mfalme.
Kusanya na Ujifunze
Kata, kunja katikati, na uhifadhi
KADI YA BIBLIA 4 ESTA
MASWALI
A. Esta aliwekwa malkia badala ya nani?
B. Kamilisha sentensi hii ya Biblia: “Esta alikuwa akizidi kupata . . .”
C. Jaza mapengo. Jina la Kiebrania la Esta lilikuwa ________, na binamu yake ________ mwenye umri mkubwa kuliko yeye akawa mlezi wake.
[Chati]
4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.
Adamu aumbwa Aliishi miaka Kitabu cha mwisho
ya 400 K.W.K. cha Biblia kinaandikwa
[Ramani]
Esta aliishi Shushani, jiji la Milki ya Muungano wa Umedi na Uajemi
UMEDI
Shushani
UAJEMI
ESTA
MAMBO MACHACHE KUMHUSU
Yatima ambaye alikuja kuwa malkia wa Mfalme Ahasuero Mwajemi. Esta alihatarisha maisha yake ili aripoti njama ya kuwaangamiza Wayahudi. (Esta 4:11, 15, 16) Sifa zake za ujasiri, busara, na roho yake ya kujitiisha zilikuwa muhimu zaidi kuliko urembo wake.—Esta 2:7; 1 Petro 3:1-5.
MAJIBU
A. Vashti.—Esta 1:12; 2:16, 17.
B. “. . . kibali machoni pa kila mtu aliyemwona.”—Esta 2:15.
C. Hadasa (linalotokana na Mhadasi), Mordekai—Esta 2:7.
Watu na Nchi
4. Jina langu ni You-Jin. Nina umri wa miaka 7 na ninaishi nchini Korea, barani Asia. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Korea? Ni 9,700, 37,900, au 96,600?
5. Ni nukta gani inayoonyesha eneo ninamoishi? Chora duara kuizunguka na utie nukta kuonyesha eneo unaloishi, kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Korea.
A
B
C
D
Watoto Watafute Picha
Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.
● Majibu ya ukurasa wa 30 na 31 kwenye ukurasa wa 15
MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
1. Mordekai hapaswi kuwa amepanda gari, anapaswa kuwa amepanda farasi wa mfalme.
2. Mordekai anapaswa kuwa amevaa mavazi ya kifalme si mavazi ya kawaida.
3. Mordekai alipita kwenye kiwanja cha watu wote si nje ya kuta.
4. 96,600.
5. D.