Wimbo 109
Uzima wa Milele Umeahidiwa
1. Mungu ameuahidi
Huo uzima hapa,
Dunia kwa ukamili.
Hayo siyo ndoto.
(Korasi)
2. Ahadi ya Mungu kweli
Wapole ndio hao,
‘Tarithi hii dunia.’
Mungu ametaka.
(Korasi)
3. Mungu atupa hakika
’Tafanya yote mapya.
Baraka zitadondoka
Mithili umande.
(Korasi)
4. Yesu ameihakiki,
Pa’diso ’tarudishwa.
Na hapo ndipo Yehova
Ataabudiwa.
(KORASI)
Inawezekana
Tuishi milele.
Ahadi ya Mungu
Itatimia.