Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 11/15 kur. 518-524
  • Kuuacha Mji wa Makimbilio Kunamaanisha Hasara ya Uhai

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuuacha Mji wa Makimbilio Kunamaanisha Hasara ya Uhai
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • HATIA YA DAMU KWA KUSHIRIKI DARAKA
  • NAMNA YA KUUKIMBILIA MJI WA MAKIMBILIO WA LEO
  • OMBI KWA MUNGU LA DHAMIRI SAFI
  • WAKATI WA KUFUNGULIWA KATIKA MJI WA MAKIMBILIO
  • Kaa Katika “Jiji la Makimbilio” Ukaishi!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Kulipiza Kisasi Juu ya Damu ya Wasio na Hatia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Je, Unamfanya Yehova Kuwa Kimbilio Lako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Majiji ya Makimbilio—Uandalizi Wenye Rehema wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 11/15 kur. 518-524

Kuuacha Mji wa Makimbilio Kunamaanisha Hasara ya Uhai

1. Kama Wayahudi wa siku za Yesu, Kristendomu yu katika hali gani?

LEO hatia ya damu iko juu ya Kristendomu na juu ya ulimwengu wote. Kwa sababu wao wenyewe hawajamwua mtu au kushiriki katika vita, watu wengi wenye mioyo minyofu hawajui kwamba wao wenyewe wanashiriki katika hatia. Walakini, inawapasa washiriki daraka hili pamoja na wale wanaofananishwa katika unabii kuwa walimwaga damu isiyo na hatia. Leo Kristendomu yu katika hali ile ile kama Wayahudi wa wakati wa Yesu, ambao Yesu aliwaambia hivi: “Angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. Amin, nawaambieni, mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki. Ee Yerusalemu Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako!”​—Mt. 23:34-37.

2. Hatia ya damu ya Yerusalemu ilitokana na nini, na alipokea patilizo (adhabu) gani?

2 Hatia ya damu ya Yerusalemu ilitokana, si na kushiriki katika vita vya kitheokrasi kwa amri ya Yehova Mungu, bali kwa sababu yeye alimwaga damu isiyo na hatia na kwa kukusudia akawaua wengi wa manabii wa Mungu, hata Yesu, Mwana wa Mungu, akihukumiwa kufa huko. Jambo hili halikufanywa bila hatia, kwa maana karne saba zilizotangulia, katika siku za Yeremia, Yehova alifunua hatia ya damu ya Yerusalemu wakati aliposema kupitia kwa nabii wake hivi: “Pia, katika marinda yako zimeonekana alama za damu ya nafsi za maskini wasio na hatia. Sikuziona katika tendo la kuvunja nyumba, lakini ziko juu ya wote hawa. Lakini wewe wasema, ‘Mimi sina hatia. Bila shaka hasira yake imeondoka kwangu.’ Tazama mimi ninashindana na wewe kwa sababu wewe unasema, ‘Mimi sikufanya dhambi.’” (Yer. 2:34, 35, NW) Akitekeleza maneno haya, katika mwaka wa 607 B.C.E. Yehova alionyesha hasira yake juu ya Yerusalemu kwa sababu ya umwagaji wake wa damu kwa kukusudia, na wafishaji wake wa Kibabeli waliimwaga damu yake chini katika uharibifu wenye kuogofya sana. Vivyo, tena, Yerusalemu alipata mauaji makubwa mengine, katika utimizo wa maneno ya Yesu, na mbele ya kumalizika katika kiangazi cha mwaka wa 70 C.E. watu 1,100,000 walikuwa wamekufa katika mji uliozingiwa.

HATIA YA DAMU KWA KUSHIRIKI DARAKA

3. Kwa sababu gani wengi ambao hawakuwa wameua uhai waliangamia?

3 Ebu zaidi wale waliomo katika Kristendomu na watii mfano huu wenye kuonya. Si Wayahudi wote waliouawa na Wababeli au na Warumi waliokuwa na hatia ya kuwaua moja kwa moja manabii wa Mungu au kwa vingine kuua uhai wa kibinadamu, hata hivyo waliangamia pamoja na wale ambao kwa kukusudia walikuwa wameimwaga damu isiyo na hatia. Kwa sababu gani hivyo? Kwa sababu waliunga mkono maandishi na mapokeo ya dini ya Kiyahudi na katika njia hiyo wakashiriki daraka hili la jamii la hatia yake ya damu.

4. Kwa sababu gani Yehova hawezi kuachilia hatia ya Kristendomu?

4 Kwa kweli Kristendomu ndio mfano wa kisasa wa Yerusalemu na makao yake ya Yuda. Hali ya Kristendomu mbele za Mungu imetiwa madoa kwa damu iliyomwagwa pasipo haki tangu mwanzo wake katika karne ya nne, katika wakati wa Konstantino. Hali hii haiwezi kuachiliwa mbali, kwa maana Yehova, asiyegeuka, alimwambia Nuhu hivi: “Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu; maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.”​—Mwa. 9:5, 6.

5. (a) Ni matendo gani ya Kristendomu ambayo yamethibitisha hatia yake, na kwa sababu gani hawawezi kujihesabia haki? (b) Ni nani wanaoshiriki hatia ya damu ya Kristendomu?

5 Mamia ya vita vya Kristendomu zaidi ya baraza za kidini za kuwahukumia wazushi wa dini na vita vya kidini mbele ya mwaka wa 1914 vimepoteza maisha za mamia ya maelfu yasiyohesabika ya watu wasio na hatia, na vita viwili vya ulimwengu tangu mwaka wa 1914, ambavyo kwa hivyo lazima Kristendomu awe na daraka kubwa juu ya makumi ya mamilioni ya maisha, vimeongeza deni kubwa ya damu, ambayo ni lazima ailipe kulingana na amri ya Mungu juu ya damu. Vita hivi haviwezi kudaiwa kuwa vita vya kitheokrasi vilivyopiganwa katika jina la Mungu, ijapokuwa makuhani na mapadre wa pande zote mbili katika mashindano haya yaliyofanywa katika Kristendomu wamewaombea washiriki wao baraka. Jambo hili halikumruhusu ye yote amwue mwanadamu mwenzake na kuwa asiye na hatia ya damu mbele za Yehova Mungu. Kuja chini ya baraka hiyo ya mapadre hakukuwa kuja katika “mji wa makimbilio” wa Kuhani Mkuu wa Yehova, Yesu Kristo. Vijapopiganwa kwa unyofu wa moyo na wengi katika bidii ya kidini au ya kupenda nchi ya kwao, kutajwa kwa jina la Mungu juu ya vita hivyo hakukuwaondolea washiriki hatia ya damu. Tena, wale wanaokubali, kusaidia au kuwaunga watu hao mkono wanaomwaga damu moja kwa moja, au kushiriki katika maenezi na shughuli hizo zinazoongoza kwenye umwagaji usio na hatia wa damu, vile vile wanakuja chini ya daraka la jamii ya watu kama washiriki wa uvunjaji wa sheria na ni lazima wasimame mbele za Mungu wa haki, asiyeweza na ambaye hataiachilia hatia hiyo ya damu.

6. Kristendomu yuna hatia ya tendo gani zaidi, na je! ataepuka adhabu ya hili?

6 Walakini, ambayo ni nzito zaidi kuliko hatia zote ni ile hatia ya damu ya Kristendomu kwa sababu ya kuua maisha za wengi wa watumishi wa kweli wa Mungu. Babeli Mkuu, milki ya ulimwenguni pote ya dini ya uongo, ambayo Kristendomu ndiyo sehemu yenye kutawala, inasimuliwa katika kitabu cha Ufunuo kama “amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.” (Ufu. 17:6) Kama vile Kristendomu amekataa kutii onyo la Yehova, vivyo karibuni hukumu ya Yehova italetwa juu yake kama ilivyoletwa juu ya mfano wake wa zamani, Yerusalemu na Yuda, katika mwaka wa 607 B.C.E. na 70 C.E. Watu wote watakaopatikana wakishirikiana naye wakati huo watakuwa washiriki katika hatia yake na ni lazima vile vile washiriki katika uharibifu wake.​—Ufu. 18:4.

NAMNA YA KUUKIMBILIA MJI WA MAKIMBILIO WA LEO

7. Ni wakati gani Mlipiza Kisasi cha damu wa Yehova atakapopiga, na ni mahali gani peke yake panapopatikana kimbilio?

7 Kwa rehema Yehova amemzuia Mlipiza Kisasi cha damu, Bwana Yesu Kristo, pamoja na majeshi yake ya kimalaika asimpige Kristendomu na wote wanaoshiriki katika hatia yake ya damu, lakini karibuni wakati huo utakwisha. (Ufu. 7:1-3) Katika “dhiki kubwa” inayokuja Mlipiza Kisasi cha damu ya kibinadamu atapiga. “Kwa maana, tazama, [Yehova] anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.” (Isa. 26:21; Mt. 24:21, 22) Wakati huo wa kuamua utakapofika, wanadamu wote watafanywa waonane na daraka lao la shirika, na hii itakuwa kwa kadiri iliyo kubwa zaidi kuliko Yerusalemu na Uyahudi. Wote ambao hawakuona mahali pa usalama watafanywa walipe adhabu. Ni lazima dunia iondolewe kabisa damu ya wale waliouawa isivyo haki. Ni lazima upatanisho ufanywe ili amri juu ya utakatifu wa damu ambayo alifanya na Nuhu ipate kutimizwa. Njia peke yake ya kuukimbilia usalama ni kutafuta barabara inayoongoza kwenye “mji wa makimbilio” wa mfano wa Yehova na kukaa humo mpaka siku ya hasira ya Yehova ipite na kuendelea kukaa ndani yake chini ya faida ya Kuhani Mkuu zaidi wa Yehova, Yesu Kristo. Basi, ni mji gani ambao ndio mji wa makimbilio uliofananishwa?

8. Ni mji gani wa kimbilio wa mfano, na kuingia humo kunafanywa namna gani?

8 Katika Israeli wa kale yampasa mwuaji aukimbilie mmojawapo wa miji sita iliyofanywa kwa kusudi hilo, na, akiisha kuthibitisha hali yake ya kutokuwa na hatia juu ya uuaji wa kukusudia, yampasa akae ndani ya mji wa makimbilio mpaka kuhani mkuu aliyekuwa akitumikia wakati huo alipokufa. (Hes. 35:9-34) Hivyo mji wa makimbilio wa mfano wapaswa uwe mpango wa Yehova wa kumlinda mtu asiuawe kwa sababu ya kuvunja amri ya Mungu juu ya utakatifu wa damu. Kuingia katika mji huo kunafanywa kwa kufika kwetu na kuendelea kuwa chini ya faida za utumishi wenye bidii wa Kuhani Mkuu wake, Yesu Kristo. Uhai mkamilifu wa kibinadamu wa Yesu, alioutoa dhabihu duniani, ulilingana na ule ambao mtu wa kwanza Adamu alijifurahisha katika paradiso ya Edeni. Yesu aliutoa uhai huu usio na dhambi katika mauti na alipofufuka na kupaa kwenye mkono wa kuume wa Mungu mbinguni yeye aliweza kutoa bei ya dhabihu ya ukombozi kwa ajili ya wazao wa Adamu wanaokufa. Kwa njia hiyo Yesu akawa Mkombozi wa wanadamu, jamaa yetu wa karibu zaidi. Kwa hiyo kutumiwa kwa faida za dhabihu hii ya ukombozi kunatutakasa sisi na hatia na kunatoa upatanisho wa wanadamu na Mungu.​—Ebr. 2:14; 10:12; Rum. 5:11; linganisha Matendo 2:37-40.

9. (a) Katika kutafuta msamaha wa Mungu, jambo gani lapaswa lifanywe na kila mvunja amri ya kimungu juu ya utakatifu wa damu? (b) Paulo anakuwa mfano namna gani?

9 Kila mvunja amri ya kimungu juu ya utakatifu wa damu, kwamba ni kwa kukusudia au bila kukusudia, yampasa atafute msamaha na kufutwa kwa dhambi zake kupitia kwa imani katika damu yenye uhai ya Kuhani Mkuu, Yesu. Yampasa aonyeshe toba la unyofu wa moyo juu ya uvunjaji wake na kwa utii aendelee kuwa chini ya mpango wa kimungu kupitia kwa Kristo, akiitumainia haki na kazi nzuri za Kuhani Mkuu. Paulo, mtume, ambaye kama Sauli wa Tarso alilitesa kundi la Kikristo, hata akitoa idhini ya kuuawa kwao, ni mfano wa wale wanaovunja amri juu ya damu. “Lakini,” anasema, “nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.” (1 Tim. 1:13) Kwa sababu Yehova kupitia kwa Kristo aliona moyo huu wa kutubu katika Sauli, mwisho ukithibitishwa kwa kazi nyingi za imani, Mlipiza Kisasi cha damu, Yesu Kristo aliyefufuka, hakumwua wakati uliofuata katika “siku ya kisasi cha Mungu wetu.” (Isa. 61:2) Yesu alipojifunua mwenyewe kwa Sauli na kufunua kutesa kwa Sauli kanisa la kweli kama kumtesa Yeye, Sauli alitubu, akageuza mwendo wake wa tendo, na tangu wakati huo alijifaidi mwenyewe na faida za dhabihu ya ukombozi, kama katika mji wa makimbilio.​—Matendo 9:1-19.

OMBI KWA MUNGU LA DHAMIRI SAFI

10. Leo mtu anatafutaje kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu?

10 Kuingia peke yake katika mji wa makimbilio wa kale kwa upande wa mwuaji asiye wa kukusudia kulikuwa hakutoshi kwa ulinzi wake. Mbele ya kuweza kuendelea kukaa katika mji na kupokea faida ambazo mji ungetoa inampasa athibitishe kwamba alikuwa ana dhamiri safi kwa Mungu kwa habari ya umwagaji wa kukusudia wa damu. Leo dhamiri safi hii kwa Mungu inaweza kupatwa kwa ombi la unyofu wa moyo tu kwa Mungu linaloonyeshwa katika kujiweka wakf kwa Mungu kupitia kwa Kristo halafu ubatizo. Hii ina maana kwamba mtu anayemfikia Mungu yampasa azikubali dhambi ambazo amefanya kwa kuvunja sheria ya Mungu na yampasa augeuze mwendo wake wa tendo kwa habari ya kufanya mapenzi ya Mungu. Kwa njia hiyo, kuweka maisha yake wakf kabisa kunapaswa kufanywe kwa Yehova kisha kujitoa mwenyewe kwa kuzamishwa kabisa katika maji kwapaswa kutukie ili kufananisha kujiweka kwake wakf. Zaidi sasa kwa vile mwisho wa ulimwengu wakaribia.

11. Dhamiri safi tunayoomba ni nini, nayo inaendelezwaje?

11 Mtume Petro alisema juu ya nguvu ya kuokoa ya ubatizo na namna unavyokamatana na dhamiri ya Kikristo wakati alipoandika katika 1 Petro 3:20, 21, NW: “Lile linalolingana na hili [yaani, kusalimika kwa Nuhu na jamaa yake gharika katika safina katika mwisho ule wa ulimwengu] pia linawaokoa ninyi sasa, yaani, ubatizo, (si kuwekewa mbali kwa uchafu wa mwili, bali ombi linalofanywa kwa Mungu kwa dhamiri njema,) kupitia kwa ufufuo wa Yesu Kristo.” Dhamiri tunayoomba kutoka kwa Mungu kwa kufuata mpango wake wa ubatizo ndiyo dhamiri isiyo na hatia yo yote kwa Mungu. Ni ufahamu wa mpango wa dhabihu ya Yesu yenye kupatanisha ndio unaotutakasa sisi sote na dhambi, si kama dhabihu za wanyama zilizopaswa zitolewe kila mwaka. Hapana, dhamiri hii njema ambayo Mungu anatupa sisi inaturuhusu tuingie katika ujamaa ulio safi na Yehova na kuendelea kuwa hivyo kwa kujifaidi wenyewe na utumishi wa Kuhani Mkuu wake. Wale wanaoingia katika hali hii inawapasa waendeleze dhamiri hiyo njema kwa kuendelea kuifanya kazi waliyogawiwa katika mji huu wa makimbilio wa mfano. Kwa hiyo dhamiri ina sehemu ya maana katika kuendelea kwetu kukaa katika mji wa makimbilio.

12. Tunawezaje kujitia wenyewe katika hatari ya kuuacha mji wa makimbilio wa kisasa?

12 Tukiisha kuingia katika mji wa mfano kupitia kwa wakf na ubatizo chini ya mpango wa dhabihu ya upatanisho ya Kristo Yesu, tunaiacha hali yote ya kujiona hatia nasi imetupasa tuendelee katika mji tukiwa na uhuru ule ule. Walakini, ikiwa tunaanza kuifanya dhamiri yetu kuwa ngumu juu ya Mungu na kujaribu kujitetea wenyewe hata kwa uvunjaji mdogo wa sheria ya Yehova inayopewa kwa wakimbizi hao waliomo katika mji, tunajiweka wenyewe katika hatari ya kuuacha mji kabisa mwishowe. Sheria ya Mungu inaelezwa waziwazi kwetu katika Neno lake na kupitia kwa vitabu vya Biblia ambavyo ametoa ili tuyafahamu mapenzi yake na kusudi lake kwa wanadamu katika wakati wa mwisho. Kutojali uongozi huu ulio wazi wa roho ya Mungu ni kutojali uongozi wa dhamiri yetu ya Kikristo. Kutojali dhamiri mwisho ni kutosikia maumivu au kusumbuliwa wakati imepaswa ituchome. Mwisho, kama Paulo alivyosema, dhamiri yaweza kufanywa kuwa ngumu kama mwili uliochomwa kwa chuma cha kuchomea. Katika hali hii dhamiri, kama kovu, haisikii maumivu, haijioni hatia. Mwisho tungeweza kuona haidhuru kufanya makosa, na wakati kosa linatajwa kwetu tutadharau kana kwamba tunasema hivi: “Halafu nini? Nani anajali?” Moyo huo wa kutojali unaweza kuongoza kwenye kutojali kabisa mpango ambao chini yake tuliruhusiwa kuingia katika mji, na tukipatwa katika hali hii, hali hii ya akili, tusingepata ulinzi kutoka kwa Mlipiza Kisasi cha damu kwa sababu tusingekuwa tena katika mji huu chini ya faida za ulinzi za Kuhani Mkuu wakati wa “siku ya kisasi” inayokuja.

13. Mtu anauacha mji wa makimbilio wa mfano namna gani, hili laweza kuepukwa namna gani, na wanapata hatari gani wale wanaouacha?

13 Kwa kuwa kugeuka kuwa mwenye kujitegemea na kupoteza imani katika dhabihu ya Kuhani Mkuu na kutotumainia tena ondoleo lake la dhambi ni kuuacha mji wa makimbilio, kwa njia hiyo kujiweka wenyewe katika hatari ya kuharibiwa katika Har–​Magedoni, itafaa tulitii onyo la mtume Paulo wakati aliposema: “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.” (Ebr. 2:1) Wakati wa Mlipiza Kisasi wa Yehova kuanza kutenda unaendelea kuwa karibu zaidi. Sasa sio wakati wa kugunduliwa, nje ya mji wa makimbilio au katika hatari karibu na ukingo wa malishoni, ulioweka mpaka wa mahali hapa pa kukimbilia palipotayarishwa na Yehova. Haitupasi kuangukia katika mtego hata kidogo wa kufikiri kwamba tunaweza kupotoka hata kidogo tu kutoka katika matakwa ya haki ya Yehova. Ni nani kati yetu awezaye kusema ni katika jambo gani ambapo mtu anakuwa mwenye kukusudia katika kutoujali mpango wa Yehova na anaacha kuwa mtu asiyetumia akili nzuri? Kumbuka aliyosema Paulo katika 1 Wakorintho 4:4: “Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni [Yehova].” Je! twaweza kusema kwamba tunamtumaini Yehova ikiwa kwa kukusudia hatujali au tunavunja amri zake alizotupa sisi? Kufikiria kuuacha mji wa makimbilio wa mfano hata kwa muda ni kumshawishi Mungu atuokoe na Mlipiza kisasi wake cha damu. Isitoshe, ikiwa ingetukia kwa mtu aliye katika hali hiyo afe sasa hivi kutokana na sababu za asili mbele ya “dhiki kubwa,” yeye ana shirika gani katika ufufuo? Haitupasi hata kidogo kuacha kuweka msingi mzuri sana katika imani, kuutegemea sana utumishi wa Kuhani Mkuu zaidi, ili wakati wa ufufuo utakapofika Mlipiza Kisasi cha damu aje atukumbuke vizuri. (Mt. 24:21, 22) Kushindwa kufanya hivyo katika huu “wakati wa mwisho” kunaweza kumaanisha kuangamia kabisa. Mtu asingekuwa na pendeleo la kuokoka “dhiki kubwa” inayokuja. Anaangamizwa.

WAKATI WA KUFUNGULIWA KATIKA MJI WA MAKIMBILIO

14. Ni mpaka wakati gani inawapasa wale walio duniani sasa ambao wana matumaini ya kimbinguni wakae ndani ya mji wa mfano, na kwa sababu gani mpaka wakati huo?

14 Ni mpaka wakati gani inawapasa wenye hatia ya damu wa zamani wakae ndani ya mji wa makimbilio? Mpaka watakapokuwa hawana haja tena na utumishi wa Kuhani Mkuu. Paulo aliwaandikia Waebrania hivi: “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu.” (Ebr. 7:25, 26) Basi, utumishi huo ni wa wale watakaookoka “dhiki kubwa” walio katika hali ya kutokukamilika kwa kibinadamu. Kwa kadiri hatia ya damu inavyoendelea, utumishi wa Kuhani Mkuu ni wa lazima ili kuendeleza hali nzuri na Mungu. Wale ambao wametiwa mafuta kwa roho takatifu ya Mungu wawe wana wa kiroho, warithi washirika na Kristo, inawapasa wawe ndani ya mji wa makimbilio wa mfano mpaka watakapoumaliza mwendo wao wa kidunia kwa uaminifu katika mauti, kwa njia hiyo wautoe milele mwili wao wa kibinadamu. Kwa kuwa dhabihu ya Kristo inatumika kwa wale walio na mwili wa kibinadamu peke yao, Kuhani Mkuu ‘anakufa’ kwao katika maana ya kwamba anakuwa hahitajiwi tena kutenda kwa ajili yao kwa wema wa dhabihu yake ya kibinadamu, kwa maana kwa habari ya “kundi dogo” la “warithio pamoja na Kristo” katika ufufuo wao wanageuzwa kutoka katika hali ya kibinadamu wanakuwa katika hali ya roho na tangu wakati huo wanakaa mbinguni wakiwa na “tabia ya Uungu.”​—Luka 12:32; Rum. 8:17; 2 Pet. 1:4.

15. Ni wakati gani wale walio na matumaini ya kidunia wanapokuwa huru kuuacha mji wa mfano, na ni jambo gani linalowatimizia hili?

15 Walakini, wale waokokaji wa “dhiki kubwa” wenye matumaini ya uzima wa kidunia hawafunguliwi katika mji wa makimbilio wakati adui za Mungu wamekwisha kuharibiwa penye Har–​Magedoni na patilizo limekwisha kufanywa kwa damu ya wale waliouawa bila hatia katika vizazi vya wanadamu. Kweli, wakati Mlipiza Kisasi cha damu hajatenda kama mfishaji wa Yehova, wale walio wa “mkutano mkubwa” huu yawapasa wawe wameyafua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. Hata hivyo, “dhiki kubwa” haiwaondolei hatia ya damu wala haiwaondolei mara hiyo dhambi walizorithi kutoka kwa Adamu. Ijapokuwa wanayo dhamiri safi kwa Mungu, inawapasa waendelee kuwa na dhamiri hii safi kwa kukaa ndani ya mipaka ya mji wa makimbilio wa mfano mpaka watakaporudishwa kwenye kukamilika kwa kibinadamu, kwa njia hiyo wasihitaji tena utumishi wa Kuhani Mkuu. Jambo hili litafika wakati gani? Wakati tu watakapokuwa wameufikia ukamilifu wa kibinadamu mwishoni mwa utawala wa miaka elfu wa Kristo atakapowakabidhi katika ukamilifu wao kwa Yehova wapate jaribu la mwisho la ukamilifu wao kulingana na kustahili kwao wenyewe. Wanapotoka katika ulinzi huu wa Kuhani Mkuu zaidi, Yesu Kristo, kwa kweli, yeye kama Kuhani Mkuu anakufa kwao, kwa maana hatahitaji tena kutenda kwa ajili yao kwa damu yenye kutakasa ya dhabihu yake.

16. Wale wanaotoka katika ufufuo wa uzima duniani wana hali gani juu ya mji wa makimbilio wa mfano?

16 Namna gani, basi, wale watakaofufuliwa wakati wa utawala wa miaka elfu wa Kristo? Je! ni lazima hawa, vile vile, waingie katika mji wa makimbilio na kukaa humo mpaka “kifo chake kuhani mkuu”? Hapana. Kwa maana hawa wamelipa adhabu kwa udhambi wao kwa kifo chao wenyewe. (Rum. 6:7) Wameachana na dhambi kwa kuingia katika kaburi la kawaida la wanadamu wote. Wakati wa kutoka kwa wafu, sasa wanasimama katika barabara inayoongoza, si katika mji wa makimbilio wa mfano, bali katika uzima wa milele. Wakiendelea katika njia hii ya uzima vile vile wao watasaidiwa na Kuhani Mkuu waufikie ukamilifu wa kibinadamu. Kushinda kwao jaribu la mwisho ukiisha kumalizika utawala wa miaka elfu wa Kristo kutawaletea vile vile kutangazwa na Yehova kuwa wenye haki na uhakikisho wa uzima usio na mwisho duniani. Walakini, kushindwa kutimiza matakwa ya Mungu yatakayotumiwa kwa wanadamu wakati huo kutawaletea hukumu ya mwisho ya kulaaniwa nao wataangamizwa milele, sawasawa na wale walioangamizwa miaka elfu iliyotangulia katika “dhiki kubwa.”

17. Kunatokea maulizo gani juu ya “kifo” cha Kuhani Mkuu?

17 Lakini, labda mtu fulani atauliza, namna gani maneno ya Paulo kwa Waebrania: “Tumaini hili tunalo kama nanga ya nafsi, lililo hakika na imara, nalo laingia ndani ya pazia, ambamo mtangulizi ameingia kwa ajili yetu, Yesu ambaye amekuwa kuhani mkuu kulingana na jinsi ya Melkizedeki milele”? (Ebr. 6:19, 20, NW) Kwa sababu gani inasemwa kwamba Yesu atakuwa Kuhani Mkuu milele ikiwa utumishi wake kama Kuhani Mkuu unamalizika kwa ulimwengu wa wanadamu mwishoni mwa miaka elfu? Ni katika njia gani yeye anaendelea kama Kuhani Mkuu milele?

18. Ni utumishi gani wa Kuhani Mkuu utakaomalizika, lakini kwa sababu gani hii haitakomesha ujamaa wake wote na wanadamu?

18 Katika mfano wa Kiyahudi kuhani mkuu alikufa kweli, kwa njia hiyo akimaliza si utumishi wake tu kama kuhani mkuu bali na uhai wake vile vile. Hii sivyo na Kuhani Mkuu zaidi, Yesu Kristo. Kweli, utumishi wake unamalizika katika njia hii wakati wanadamu wanapoletwa katika hali kamilifu katika haki mbele za Yehova, lakini Yesu katika mkono wa kuume wa Yehova anaendelea milele. Kukoma kwa kazi yake kama Kuhani Mkuu mwenye kupatanisha kwa wanadamu hakukomeshi uhai wake. Matokeo mema ya utumishi wake kama Mfalme na Kuhani Mkuu juu ya wanadamu yataendelea milele na wanadamu, watakuwa na deni milele kwake kwa vile atakuwa ametumikia kwa ajili yao kama Mfalme na Kuhani Mkuu. Kwa umilele wote watalipigia magoti jina la Yesu na kukiri kwamba yeye ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba. (Flp. 2:5-11) Wakati huo utumishi wake kwa wanadamu hautakuwa wa lazima tena katika kutumiwa kwa dhabihu yake yenye kupatanisha kwao. Lakini kama Msimamizi mkuu na Mneni wa Yehova, yeye bila shaka ataendelea katika umilele wote kama Yeye anayewapita wote katika kukuza sifa ya Yehova na kuongoza katika ibada itakayounganisha ulimwengu mzima kwa utukufu na heshima ya Yehova.

19. Sasa ni kitu gani kinachoweza kututegemeza sisi, na jitihada yetu ya moyo imepaswa iweje?

19 Lo! namna litakavyokuwa pendeleo lenye baraka kuwa kati ya viumbe hivyo vyenye furaha ambavyo vitakuwa vimeendelea kuishi mpaka wakati huo! Lo! namna tutakavyokuwa wenye shukrani kwa rehema ya Yehova ambayo imewezesha mpango huu wa ajabu! Ni tumaini hili sasa ndilo liwezalo kututegemeza sisi. Na tulione kuwa bora kama vile tunavyouona uhai wenyewe kuwa bora sana, kwa maana kuendelea kuwa katika mji wa makimbilio wa Yehova sasa katika huu “wakati wa mwisho” wa ulimwengu wenye hatia ya damu kunamaanisha uhai wetu.

​—Kutoka The Watchtower, May 15, 1973.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki