HAZINA ZA NENO LA MUNGU | KUTOKA 25-26
Kitu Muhimu Zaidi Katika Hema la Ibada
Kitu muhimu zaidi katika hema la ibada na katika kambi yote ya Israeli kilikuwa Sanduku la Agano. Kuwapo kwa Mungu kuliwakilishwa na wingu lililokuwa katikati ya makerubi wawili waliokuwa juu ya kifuniko cha Sanduku hilo. Siku ya Kufunika Dhambi ya kila mwaka, kuhani mkuu aliingia ndani ya Patakatifu Zaidi na kunyunyiza damu ya ng’ombe dume na ya mbuzi mbele ya kifuniko ili kufunika dhambi za Waisraeli. (Law 16:14, 15) Hilo lilitangulia kuonyesha jinsi ambavyo Yesu, yule Kuhani Mkuu zaidi, atakavyoingia mbele ya kuwapo kwa Yehova mbinguni ili kutoa thamani ya dhabihu yake ya fidia.—Ebr 9:24-26.
Patanisha maandiko yafuatayo na manufaa tunazoweza kupata kutokana na fidia:
MAANDIKO
MANUFAA
tumaini la kuishi milele
msamaha wa dhambi
dhamiri safi
Tunapaswa kufanya nini ili kupokea manufaa hayo?