14 Basi akayavua mavazi ya ujane wake, akavaa shali na kujifunika uso, naye akaketi chini kwenye mwingilio wa Enaimu, jiji lililo katika barabara inayokwenda Timna. Kwa maana aliona ya kwamba Shela alikuwa ameshakuwa mtu mzima na bado hakuwa amekabidhiwa kwake awe mke wake.+