Maelezo ya Chini
i Ndugu Rutherford aliacha mke, Mary, na mwana wao, Malcolm. Kwa sababu Dada Rutherford alikuwa na afya mbaya na aliona majira ya baridi katika New York (yalipokuwa makao makuu ya Watch Tower Society) kuwa magumu kuvumilia, yeye na Malcolm walikuwa wakikaa katika sehemu ya kusini mwa California, ambako hali ya hewa iliifaa zaidi afya yake. Dada Rutherford alikufa Desemba 17, 1962, akiwa na umri wa miaka 93. Tangazo la kifo chake lililotokea katika Daily News-Post la Monrovia, California, lilitaarifu hivi: “Mpaka afya yake mbaya ilipomzuia kutoka nyumbani mwake, yeye alishiriki kwa bidii katika kazi ya kihuduma ya Mashahidi wa Yehova.”