Maelezo ya Chini
c Simulizi hilo linatoa mifano miwili ya ukosefu wa heshima. Kwanza, Sheria ilitaja kihususa vipande vya nyama vilivyotolewa dhabihu ambavyo makuhani waliruhusiwa kula. (Kum. 18:3) Lakini katika maskani, makuhani hao waovu walifanya jambo tofauti kabisa. Waliwalazimisha wahudumu wao kuingiza uma mkubwa ndani ya chungu cha kupikia ambacho kilikuwa na nyama zilizokuwa zikitokota, na kutoa kipande chochote kizuri walichopata! Pia, watu walipoleta dhabihu zao ili ziteketezwe juu ya madhabahu, makuhani hao waovu waliwatuma wahudumu kuwasumbua watu kwa kuwaambia wawape nyama mbichi kabla ya kumtolea Yehova dhabihu ya sehemu ya mafuta.—Law. 3:3-5; 1 Sam. 2:13-17.