Maelezo ya Chini
a Apokrifa (kihalisi lamaanisha, “kilichofichwa”) na Pseudepigrapha (kihalisi lamaanisha, “maandishi yaliyodhaniwa kimakosa kuandikwa na mtu fulani”) ni maandishi ya Wayahudi yaliyoandikwa kuanzia karne ya tatu K.W.K. hadi karne ya kwanza W.K. Kanisa Katoliki limekubali Apokrifa kuwa sehemu ya maandiko ya Biblia yaliyopuliziwa na Mungu, lakini Wayahudi na Waprotestanti wamekataa vitabu hivyo. Vitabu vingi vya “Pseudepigrapha” vina maelezo ya ziada kuhusu masimulizi ya Biblia, na yasemekana viliandikwa na baadhi ya watu mashuhuri wa Biblia.