-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
kulisimamishwa. (Ufunuo 11:7-10) Hiyo ilikuwa wakati walipopatwa na kituko kama kile cha Waisraeli katika Misri ambao pia walivumilia chini ya uonevu mkubwa. Ikawa ndipo Yehova alipowaleta upesi, kama kwa mabawa ya tai, kwenye usalama katika jangwa la Sinai. (Kutoka 19:1-4) Hali kadhalika, baada ya mnyanyaso mkali wa 1918-19, Yehova alikomboa mashahidi wake, wenye kuwakilisha mwanamke wake, akawaingiza ndani ya hali ya kiroho iliyokuwa salama kwao kama jangwa lilivyokuwa kwa Waisraeli. Hiyo ilikuja ikiwa jibu la sala zao.—Linga Zaburi 55:6-9.
25. (a) Ni nini alichotokeza Yehova katika 1919, kama alivyotokeza Waisraeli wakiwa taifa jangwani? (b) Ni nani wanaojumlika kuwa taifa hili, nao wameletwa ndani ya nini?
25 Huko jangwani, Yehova aliwatokeza Waisraeli wakiwa taifa, akiwaandalia kiroho na kimwili. Hali moja na hiyo, kuanzia 1919, Yehova aliitokeza mbegu ya mwanamke ikiwa taifa la kiroho. Hili lisifikiriwe kuwa ule Ufalme wa Kimesiya ambao umekuwa ukitawala kutoka katika mbingu tangu 1914. Badala ya hivyo, washiriki wa hili taifa jipya ni baki la mashahidi wapakwa-mafuta walio duniani, walioletwa ndani ya hali ya kiroho tukufu katika 1919. Wakiwa sasa wanaandaliwa “kipimo cha ugavi wa chakula chao kwa wakati unaofaa,” hao waliimarishwa kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele.—Luka 12:42, NW; Isaya 66:8.
26. (a) Kile kipindi cha wakati kinachotajwa kwenye Ufunuo 12:6, 14 ni cha urefu gani? (b) Ni nini lililokuwa kusudi la kipindi hicho cha nyakati tatu na nusu, kilianza lini na kilikwisha lini?
26 Pumziko la muda hili la mbegu ya mwanamke wa Mungu lilidumu kwa muda gani? Ufunuo 12:6 husema siku 1,260. Ufunuo 12:14 hukiita kipindi hicho wakati, nyakati, na nusu wakati; kwa maneno mengine, nyakati tatu na nusu. Kwa kweli, semi zote mbili husimamia miaka mitatu na nusu, ikiendelea katika Kizio cha Kaskazini kutoka masika ya 1919 kufika vuli ya 1922. Hiki kilikuwa kipindi cha ponyo lenye kuburudisha na kujipanga tena kitengenezo kwa jamii ya Yohana iliyorudishwa.
27. (a) Kulingana na ripoti ya Yohana, yule drakoni alifanya nini baada ya 1922? (b) Ni nini lililokuwa kusudi la Shetani kutapika nje furiko la mnyanyaso dhidi ya Mashahidi?
27 Yule drakoni hakuchoka! “Na drakoni akatapika maji kama mto kutoka kinywa chake baada ya mwanamke, ili kufanya yeye azamishwe na mto.” (Ufunuo 12:15, NW) Ni nini kinachomaanishwa na “maji kama mto,” au “furiko la maji”? (The New English Bible) Mfalme Daudi wa kale alisema juu ya waovu ambao walimpinga kuwa “mafuriko-bubujiko ya watu wasiofaa kitu [“vijito vya wasio na thamani,” Young]. (Zaburi 18:4, 5, 16, 17, NW) Hali kadhalika, anachofungulia Shetani ni kunyanyaswa na wasio na thamani au “watu wasiofaa kitu.” Baada ya 1922 Shetani alitapika furiko la mnyanyaso dhidi ya Mashahidi. (Mathayo 24:9-13) Hilo lilikuja kutia ndani jeuri ya kimwili, “kutunga matata kwa amri,” vifungo, na hata kunyongwa kwa kutundikwa, kupigwa risasi, na kukatwa kichwa. (Zaburi 94:20, NW) Shetani aliyetwezwa, akiwa amenyimwa ruhusa ya kumfikia moja kwa moja mwanamke wa Mungu, alianza kushambulia kwa hasira-kisasi ile mbegu yake inayobaki duniani na kuwaangamiza, ama moja kwa moja ama kwa kusababisha wapoteze kibali cha Mungu kwa kuvunja ukamilifu wao. Lakini azimio lao lilithibitika kuwa kama lile la Ayubu: “Mpaka mimi niishe mimi sitaondolea mbali ukamilifu wangu kutoka kwangu mwenyewe!”—Ayubu 27:5, NW.
28. Furiko la mnyanyaso lilifikiaje kilele wakati wa Vita ya Ulimwengu 2?
28 Furiko hili la ukatili la mnyanyaso lilifikia kilele wakati wa Vita ya Ulimwengu 2. Katika Ulaya Mashahidi wapatao 12,000 walitiwa katika kambi za mateso za Nazi, na 2,000 hivi wakafa. Chini ya mabwana wa vita waliotawala Italia, Japani, Korea, na Taiwani, Mashahidi waaminifu walipata kutendewa kikatili vivyo hivyo. Hata katika yale mabara yanayoitwa eti ya kidemokrasi, Mashahidi walishambuliwa na vikundi vya Aksio Katoliki, wakapakwa lami na kuvikwa manyoya, na wakafukuzwa kutoka mji. Makusanyiko ya Wakristo yalivunjwa na watoto wa Mashahidi wakafukuzwa shuleni.
29. (a) Yohana anaelezaje habari ya muawana ukiwasili kutoka chimbuko lisilotazamiwa? (b) “Dunia ikaja kusaidia mwanamke” jinsi gani? (c) Yule drakoni alieendelea kufanya nini?
29 Muawana uliwasili kutoka chimbuko lisilotazamiwa: “Lakini dunia ikaja kusaidia mwanamke, na dunia ikafungua kinywa chayo na ikameza kabisa mto ambao yule drakoni alitapika kutoka kinywa chake. Na drakoni akajaa hasira-kisasi kuelekea mwanamke, na akatoka kwenda kufanya vita na wabakio wa mbegu yake, ambao hushika amri za Mungu na wana kazi ya kutoa ushahidi kwa Yesu.” (Ufunuo 12:16, 17, NW) “Dunia”—elementi zilizo ndani ya mfumo wa mambo wa Shetani mwenyewe—ikaanza kumeza ule “mto,” au “furiko.” Wakati wa miaka ya 1940 Mashahidi walianza kupata mfululizo wa maamuzi yenye kupendeleka katika Mahakama Kuu Zaidi Sana ya United States, na kutoka mamlaka zenye kutawala katika mabara fulani, ambayo yalitetea uhuru wa ibada. Mwishowe, Mataifa-Mafungamani yakameza kabisa hiyo kani kubwa gandamizi ya Kinazi-Fashisti, kwa kuauni Mashahidi ambao walikuwa wameteseka chini ya tawala katili za kidikteta. Minyanyaso haikukoma kabisa, kwa kuwa yule drakoni ameendelea mpaka leo hii, naye huendeleza vita dhidi ya wale ambao “wana kazi ya kutoa ushahidi kwa Yesu.” Katika mabara mengi, Mashahidi washikamanifu wangali wamo gerezani, na baadhi yao wangali wanakufa kwa sababu ya ukamilifu wao. Lakini katika mengine ya mabara haya, wakati kwa wakati wenye mamlaka hulegeza mbano wao, na Mashahidi hufurahia kipimo kikubwa zaidi cha uhuru.c Hivyo, katika utimizo wa unabii, dunia huendelea kumeza mto wa mnyanyaso.
30. (a) Dunia imeandaa muawana wa kutosha kwa ajili ya kitu gani kitukie? (b) Ukamilifu wa watu wa Mungu hutokeza nini?
30 Katika njia hii, dunia imeandaa muawana wa kutosha kuruhusu kazi ya Mungu iendelee kwenye mabara 235 hivi na kuzaa wahubiri wa habari njema waaminifu zaidi ya milioni sita. Pamoja na wabakio wa mbegu ya mwanamke, umati mkubwa wa kimataifa wa waumini wapya unashika amri za Mungu kwa habari ya kujitenga na ulimwengu, adili safi, na upendo kwa akina ndugu, na wao wanashuhudia Ufalme wa Kimesiya. Ukamilifu wao unajibu shtaka lenye suto la Shetani, hivi kwamba onyo la kifo linavumishwa kwa ajili ya Shetani na mfumo wake wa mambo.—Mithali 27:11.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Sura ya 28
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
Njozi ya 8—Ufunuo 13:1-18
Habari: Hayawani-mwitu mwenye vichwa saba, hayawani-mwitu mwenye vichwa viwili, na mfano wa hayawani-mwitu
Wakati wa utimizo: Kutoka siku ya Nimrodi hadi dhiki kubwa
1, 2. (a) Yohana anasema nini juu ya drakoni? (b) Yohana kwa lugha ya ufananisho, huelezaje habari ya tengenezo lionekanalo linalotumiwa na drakoni?
YULE drakoni mkubwa ametupwa chini kwenye dunia! Funzo letu juu ya Ufunuo limedhihirisha kwamba Nyoka au wafuasi wake roho waovu hawataruhusiwa tena kamwe warudi ndani ya mbingu. Lakini hatujamaliza habari ya “mmoja ambaye huitwa Ibilisi na Shetani, ambaye anaongoza vibaya dunia nzima yote inayokaliwa.” Simulizi linafuata kutambulisha kirefu njia anayotumia Shetani kupiga vita dhidi ya ‘mwanamke na mbegu yake.’ (Ufunuo 12:9, 17, NW) Yohana anasema hivi juu ya drakoni huyo wa kinyoka: “Na huyo akasimama tuli juu ya mchanga wa bahari.” (Ufunuo 13:1a, NW) Kwa hiyo acheni sisi tutue na kuchunguza njia ya utendaji ya huyo drakoni.
2 Mbingu takatifu hazisumbuliwi tena na kuwapo kwa Shetani na roho waovu wake. Hao roho waovu wamekwisha fukuzwa nje ya mbingu na kufungiwa kwenye ujirani wa dunia. Hapana shaka hii ndiyo sababu ya ukuzi mkubwa mno wa mazoea ya uwasiliano na roho nyakati hizi. Nyoka mwenye hila angali anadumisha tengenezo la roho lenye ufisadi. Lakini je! yeye pia anatumia tengenezo linaloonekana ili kuongoza vibaya aina ya binadamu? Yohana hutuambia hivi: “Na mimi nikaona hayawani-mwitu akipanda kutoka bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake mataji kumi, lakini juu ya vichwa vyake majina yenye kufuru. Sasa hayawani-mwitu ambaye mimi niliona alikuwa kama chui,
-