-
UtanguliziJinsi ya Kupata Maisha Yenye Kuridhisha
-
-
Utangulizi
Hebu fikiria hali hizi zinazotofautiana: Katika nchi moja ambayo imeendelea, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaona kwamba wana furaha nyingi ama wana furaha ya kiasi fulani. Lakini kati ya aina 10 za dawa zinazotumiwa sana katika nchi hiyo, aina 3 ni za kutibu ugonjwa wa kushuka moyo. Katika nchi hiyohiyo, asilimia 91 ya watu huona maisha yao ya familia kuwa yenye kuridhisha. Lakini, karibu nusu ya watu waliofunga ndoa katika nchi hiyo hutalikiana!
Utafiti uliohusisha watu katika nchi 18, ambazo zina karibu nusu ya idadi ya watu wote ulimwenguni, ulionyesha kwamba “ulimwenguni kote watu wana shaka kuhusu wakati ujao.” Basi, ni wazi kwamba watu wengi hawaishi maisha yenye kuridhisha kikamili. Namna gani wewe? Broshua hii imetayarishwa ikusaidie kufanya maisha yako yawe yenye kuridhisha kwelikweli.
-