-
Safina ya Noa na Uundaji wa MeliAmkeni!—2007 | Januari
-
-
Mungu alimwambia Noa ajenge safina yenye urefu wa mikono 300, upana wa mikono 50, na kimo cha mikono 30. (Mwanzo 6:15) Kulingana na makadirio ya watu fulani, hilo lina maana kwamba safina ilikuwa na urefu wa meta 134, upana wa meta 22, na kimo cha meta 13 hivi.a
-
-
Safina ya Noa na Uundaji wa MeliAmkeni!—2007 | Januari
-
-
Uwezo Mzuri wa Kuelea
Urefu wa safina ulikuwa mara sita zaidi ya upana wake na mara kumi zaidi ya kimo chake. Meli nyingi za kisasa zina vipimo kama hivyo, ingawa mara nyingi tofauti kati ya urefu na upana wake huamuliwa kwa kutegemea nguvu zinazohitajika ili meli isonge majini. Kwa upande ule mwingine safina ilihitaji tu kuelea. Uwezo wake wa kuelea ulikuwaje?
Uwezo wa chombo cha majini kukabiliana na upepo na mawimbi unahusiana sana na upatano katika vipimo vyake. Biblia inafafanua mvua kubwa iliyotokeza Gharika na pia inasema kwamba baadaye Mungu alitokeza upepo. (Mwanzo 7:11, 12, 17-20; 8:1) Maandiko hayasemi kuhusu nguvu ya mawimbi na upepo uliovuma lakini inawezekana kwamba yalikuwa yenye nguvu na yenye kubadilika-badilika, kama ilivyo leo. Upepo ukivuma kwa muda mrefu na kwa nguvu sana mawimbi huinuka zaidi na kusukumwa mbali zaidi. Isitoshe, utendaji wowote chini ya bahari ungeweza kutokeza mawimbi makubwa.
Vipimo vyenye upatano vya safina viliisaidia iwe imara. Vilevile safina iliundwa kwa njia ambayo ingeweza kukabiliana na nguvu ambazo zingeiinua na kuifanya ipige maji kwa mbele au nyuma wimbi linapopita. Halingekuwa jambo lenye kustarehesha kwa watu na wanyama iwapo wimbi lingeinua upande mmoja wa safina na kuiruhusu ipige maji kwa nguvu. Kupiga maji kwa njia hiyo hutahini uimara wa chombo. Chombo kinapaswa kuwa na nguvu za kutosha ili kisijipinde upande wa chini iwapo mawimbi mawili makubwa yangeinua miisho yote miwili kwa wakati uleule. Hata hivyo, wimbi kubwa linapoinua sehemu ya katikati ya chombo bila kuwa na kitu cha kushikilia miisho yake, huenda omo na tezi zikajipinda. Mungu alimwambia Noa ajenge safina kwa kutumia urefu unaozidi kina kwa mara 10. Baada ya mikasa mingi, watengeneza-meli wa baadaye walijifunza kuwa vipimo hivyo vinaweza kuhimili mikazo hiyo.
-