-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
Basi akamwachilia. Ndipo akasema: ‘Bwana-arusi wa damu,’ kwa sababu ya tohara.” (Kutoka 4:20, 24-26)
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
Maneno haya ya Sipora “wewe ni bwana-arusi wa damu kwangu” si ya kawaida. Yanaonyesha nini kumhusu Sipora? Kwa kukubaliana na matakwa ya agano la tohara, Sipora alikubali kuingia katika uhusiano wa agano pamoja na Yehova. Baadaye, agano la Sheria lililofanywa pamoja na Waisraeli lilionyesha kwamba katika uhusiano wa agano, Yehova anaweza kuonwa kuwa mume huku yule anayefanya agano naye akionwa kuwa mke. (Yeremia 31:32) Kwa hiyo, alipomtaja Yehova (kupitia malaika wake aliyemwakilisha) kuwa “bwana-arusi wa damu,” yaonekana Sipora alikuwa akikubali kutii matakwa ya agano hilo. Ilikuwa kana kwamba alikuwa amekubali kuwa mke katika agano la tohara, huku Yehova Mungu akiwa mume. Vyovyote vile, kwa sababu ya tendo lake muhimu la kutii takwa la Mungu, maisha ya mwana wake hayakuwa hatarini tena.
-