-
Kitu Chenye Thamani Zaidi Kuliko Hazina za MisriMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
Punde si punde, Miriamu alikuwa kando yake. ‘Je, nikakwitie mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kukunyonyeshea mtoto huyu?’ akauliza. Watu fulani huona taarifa hii kuwa inapingana. Dada yake Musa anatenda kinyume na Farao, aliyepanga njama na washauri wake kuwatendea Waebrania “kwa akili.”
-
-
Kitu Chenye Thamani Zaidi Kuliko Hazina za MisriMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 11]
Mapatano na Akina Mama Walioajiriwa Kunyonyesha
Kwa kawaida akina mama waliwanyonyesha watoto wao. Hata hivyo, msomi Brevard Childs asema hivi katika Journal of Biblical Literature, “nyakati fulani familia za kifalme [nchi za Mashariki ya Kati] ziliajiri mama wa kunyonyesha. Desturi hiyo ilikuwa ya kawaida wakati ambapo mama hakuweza kumnyonyesha mtoto wake au wakati ambapo mama hakujulikana. Mama wa kunyonyesha alichukua jukumu hilo la kumlea mtoto na vilevile kumnyonyesha kwa kipindi hususa.” Hati kadhaa za mafunjo zinazoonyesha mapatano yaliyofanywa na akina mama wa kunyonyesha zimepatikana katika mabaki ya vitu vya kale huko Mashariki ya Kati. Hati hizo zinathibitisha desturi hiyo iliyokuwa imeenea sana kuanzia utawala wa Wasumeria hadi mwisho-mwisho wa utawala wa Wagiriki huko Misri. Mambo yanayotajwa katika hati hizo yanatia ndani taarifa za wahusika, kipindi cha kunyonyesha, hali za kazi, chakula walichopaswa kula, faini ambayo mtu angelipa kwa kuvunja mapatano, mishahara, na jinsi ambavyo mishahara ingelipwa. Kwa kawaida, “utunzaji uliendelea kwa muda unaozidi miaka miwili hadi mitatu,” asema Childs. “Mama wa kunyonyesha alimlea mtoto nyumbani mwake, lakini nyakati nyingine alipaswa kumrudisha mtoto kwa mwenyewe ili achunguzwe.”
-