-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
4. Kwa maneno yako mwenyewe, ungeelezaje yale yanayosemwa na Zaburi 133 kuhusu muungano wa kidugu?
4 Mtunga-zaburi Daudi alithamini sana muungano wa kidugu. Hata alipuliziwa kuimba juu yao! Ebu mwazie akiwa na kinubi chake huku akiimba: “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja [“muungano,” NW]. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Heremoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, naam, uzima hata milele.”—Zaburi 133:1-3.
-
-
Familia ya Yehova Hufurahia Muungano Wenye ThamaniMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
-
-
5. Kwa msingi wa Zaburi 133:1, 2, ni ulinganifu gani uwezao kufanywa kati ya Waisraeli na watumishi wa Mungu wa siku ya sasa?
5 Maneno hayo yalihusu muungano wa kidugu uliofurahiwa na watu wa Mungu wa kale, Waisraeli. Walipokuwa Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu zao tatu za kila mwaka, kwa kweli wao walikaa pamoja kwa muungano. Ingawa walitoka makabila mbalimbali, walikuwa familia moja.
-