-
Je, Unawaburudisha Wengine?Mnara wa Mlinzi—2007 | Novemba 15
-
-
Je, Unawaburudisha Wengine?
KATIKA ncha ya kusini ya Milima ya Anti-Lebanon, kuna Mlima Hermoni ambao una kilele kilichoinuka mita 2,814 juu ya usawa wa bahari. Kilele cha Hermoni kinafunikwa na theluji kwa muda mrefu kila mwaka, na hivyo mvuke wenye joto unaopita juu ya mlima huo wakati wa usiku unaganda na kutokeza umande. Umande huo unashuka juu ya misonobari na miti ya matunda iliyo katika miteremko ya chini na pia unashuka kwenye mashamba ya mizabibu yaliyo chini hata zaidi. Katika majira marefu ya kiangazi katika Israeli la kale, umande kama huo wenye kuburudisha ndio uliokuwa chanzo kikuu cha unyevunyevu kwa ajili ya mimea.
Katika wimbo ulioongozwa na roho, umoja wenye kuburudisha wa waabudu wa Yehova unafananishwa na “umande wa Hermoni unaoshuka kwenye milima ya Sayuni.” (Zaburi 133:1, 3) Kama tu Mlima Hermoni unavyoandalia mimea umande wenye kuburudisha, ndivyo sisi tunavyoweza kuwaburudisha wale tunaokutana nao.
-
-
Je, Unawaburudisha Wengine?Mnara wa Mlinzi—2007 | Novemba 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 16]
Umande wa Mlima Hermoni —chanzo chenye kuburudisha cha unyevunyevu kwa ajili ya mimea
-