-
Tembea Katika ‘Njia ya Unyofu’Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
-
-
“Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; uangamivu wa maskini ni umaskini wao.
-
-
Tembea Katika ‘Njia ya Unyofu’Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
-
-
Kama vile mji uliozingirwa kwa ukuta huandaa usalama wa kiasi fulani kwa watu wanaoishi humo, ndivyo mali inavyoweza kuwa ulinzi dhidi ya mambo fulani maishani yanayoweza kutokea pasipo kutarajiwa. Na umaskini unaweza kutokeza madhara, mambo fulani yasiyotarajiwa yanapotokea. (Mhubiri 7:12) Hata hivyo, yaelekea mfalme huyo mwenye hekima alikuwa anadokeza hatari fulani inayoweza kusababishwa na utajiri na vilevile umaskini. Huenda tajiri akawa na mwelekeo wa kutumaini sana mali zake, akifikiri kwamba vitu vyake vyenye thamani ni “kama ukuta mrefu.” (Mithali 18:11) Na huenda maskini akadhani kimakosa kwamba umaskini humkosesha tumaini la wakati ujao. Hivyo, wote wawili wanakosa kujifanyia jina zuri pamoja na Mungu.
-